Posts

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI UGANDA-TANZANIA WAFIKIA ASILIMIA 29.

Image
  Na Al odia Babara, Bukoba Mradi wa bomba la mafuta ghafi unaotekelezwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani  Tanga nchini Tanzania umefikia asilimia 29. Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya  sh.trilioni 8 ulisainiwa mkataba wake mwaka 2021 kati ya Rais wa Uganda Yowel Kaguta Museven pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi unaendelea kutekelezwa na umefikia asilimia 29. Afisa katika kitengo cha mawasiliano bomba la mafuta EACOP Abass Abraham akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Kagera June 03, mwaka huu juu ya mwongozo kuhusu mradi wa bomba hilo amesema kuwa, hadi sasa mabomba yaliyopokelewa ni ya kusambaza umbali wa kilomita 500 na kituo cha kupokea mabomba na kuyaboresha kiko mkoa wa Tabora. "Asilimia 80 ya bomba la mafuta ziko nchini Tanzania na asilimia 20 ziko upande wa Uganda, kwa Uganda ni kilomita 296 na upande wa Tanzania ni kilomita 1,147 bomba litapita katika wilaya nane"amesema Abraham Abraham am...

KESI YA WANANDOA KUJERUHI JIRANI YAPIGWA KALENDA

Image
  Na Mwandishi Wetu SHAHIDI wa upande wa mashitaka, Kiran Lalit Ratilal, ameshindwa kutoa ushahidi katika kesi  ya kujeruhi inayowakabili wanandoa Bharat Nathwan (57) na Sangita Bharat (54), kwa sababu wakili wa utetezi katika kesi hiyo yupo Mahakama ya Rufani kwenye shauri lingine. Wanandoa hao ambao ni raia wa Tanzania wenye asili ya kihindi wanaoishi Mtaa wa Mrima - Kisutu, jengo la Lohana Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashitaka manne likiwemo la kujeruhi waliyoyatenda Julai 21,2023 kinyume cha sheria. Kesi hiyo ililetwa jumatatu tarehe 3 Juni mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka, mashahidi watatu wameshatoa ushahidi wao. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga alidai kuwa wana shahidi mmoja na wapo tayari kuendelea na ushahidi, baada ya kudai hayo, upande wa utetezi ulidai kuwa ni kweli kesi ipo kwenye hatua ya ushahidi, lakini kwa bahati mbaya siku ...

WADAU WA USHIRIKA WATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA 

Image
  Na Mwandishi wetu, Lindi. Kuelekea siku ya jukwaa la ushirika linalotarajiwa kufanyika hapo kesho juni 04, 2024 wadau wa ushirika Mkoa wa Lindi wamekabidhi misaada mbalimbali ya kibinaadamu kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Ruangwa pamoja na kupanda miti hospitalini hapo Misaada hiyo iliyokabidhiwa ni pamoja na sabuni za unga pamoja na sukari ambavyo vimegawiwa kwa akina Mama waliojifungua katika hospitali hiyo Akizungumza na Waandishi wa Habari, Bi. Cesilia Socitenes amesema kuwa huduma zilizofanyika katika Hospitali ni moja ya utekelezaji wa misingi Saba ya ushirika ambapo msingi wa saba unaelekeza kuijali jamii. Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa msingi huo wa Saba, wanachama wa Vyama vya Ushirika watachangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi ambao matibabu yao yanauhitaji wa damu. Kwa upande wake, Ndg. Richard Zengo, Mrajisi Msaidizi anayesimamia Sehemu ya Vyama Visivyo vya Kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika amesema kuwa moja ya mal...

JELA MIAKA 50, KWA UBAKAJI, WIZI NA UHUJUMU UCHUMI.

Image
  Na Mwandishi wetu, Lindi Mahakama ya hakimu mkazi Lindi chini ya hakimu mkazi mfawidhi consolata singano imewahukumu kazili kafanya  mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa dare es salaam na jonh mondo  maarufu kama kikwete kwa jina  la utapeli mwenye umri wa miaka 55 mkazi wa msavu mororgoro kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka na kwenda jela miaka 20 kwa kosa linguine la utakatishaji fedha. Hili ni shauri  la uhujumu uchumi namba tatu la mwaka 2022 ambapo kulikua na  jumla ya mashahidi 32 kutoka mikoa ya lindi, mtwara, Ruvuma, dar es salaam, Dodoma na morogoro  na vielelezo 35. Kesi hii ilikua chini ya hakimu mkazi mfawidhi  consolata singano ambapo upande wa jamuhuri ukiongozwa na wakili wa serikali godfrey mramba  ambapo ameiambia mahakama yakwamba watuhumiwa walifanya vitendo vya uzalilishaji wa kingono kwa kuwaingilia wanawake wawilia  bila ridhaa yao na kuwasababishia hasara kiuchumi kwa kuwaibia kiasi hicho cha fedha huku upande...

WIZI WA MTOTO MWENYE UALBINO MULEBA, WATATU WAKAMATWA.

Image
  A lodia Babara,  Muleba, Noela Asimwe Novath mtoto mwenye umri wa miaka miwili na nusu mwenye ualibino  ameibwa katika mikono ya mama yake baada ya mtu mmoja  asiyejulikana kupiga hodi nyumbani kwao na kuomba msaada wa chunvi akidai amenga’twa na nyoka katika kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu  wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Mama mzazi wa mtoto huyo Judith Richard amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 30, mwaka huu saa 7:30 jioni wakati mama huyo akiwa amekaa ndani na mtoto wake ndipo mtu huyo alipokuja na kupiga hodi bila kutaja jina lake na kusema kuwa, amenga’twa na nyoka hivyo  anaomba msaada wa chunvi. Judith amefungua mlango na kumuona mtu ambaye alikuwa akitembea kwa kuchechemea bila kujua kumbe alikuwepo mtu mwingine amejibanza  ukutani ambapo aliyekuwa amejibanza ukutani alimkaba koo na aliyekuwa anachechemea  aliingia ndani na kutokomea na mtoto kusikojulikana.  “Kuna mtu alipiga hodi aka...

NMB YATOA MSAADA VIFAA TIBA VYA MILIONI 10 HOSPITALI YA BAGAMOYO

Image
  Benki ya NMB yatoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni kutekeleza majukumu yao ya kusaidia wananchi katika kuimarisha afya zao. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Meneja wa kanda ya Dar es salaam, Ferdinand Mpona, amesema NMB imetekeleza msaada huo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali chini ya uongozi wake Dkt. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda, amesema wanaishukuru Benki ya NMB kwa kutoa vifaa hivyo kwani vitasaidia katika matibabu ya afya za wananchi. Amesema serikali imetenga fedha za kujenga na kukarabati majengo mbalimbali ya Hospitali ya Bagamoyo hivyo inapokea taasisi binafsi zikajitolea kusaidia vifaatiba inasaidia kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Vitanda vitano vya kujifungulia kinamama wajawazito, pamoja na magodoro yake, na viti vya magurudu...

DED BAGAMOYO AFUNGUA MAFUNZO KUHUSU MABORESHO YA MITAALA YA ELIMU YA AWALI, MSINGI, SEKONDARI NA UALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI BAGAMOYO MKOANI PWANI.

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw Shauri Selenda tarehe 30 Mei 2024 amefungua mafunzo kuhusu maboresho ya mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo Mkoani Pwani. Mafunzo hayo, yamelenga kuwapitisha washiriki katika muundo wa Elimu, Maboresho Elimu Msingi na Sekondari pamoja na Ualimu. " Ndugu zangu nyinyi mliopo hapa ni asilimia ndogo sana ya washiriki wanaohitajika kupata mafunzo haya, hivyo nawaomba muwe makini kutumia muda Ili muweze kupata Yale yaliyotarajiwa kutoka kwa wawezeshaji wetu ". Alisema Bw Selenda. Mafunzo haya ya siku mbili  yanajumuisha Walimu Wakuu 78 toka Shule za Msingi za Serikali na binafsi Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Ofisi ya Raisi- TAMISEMI