Na Mwandishi wetu, Lindi
Hili ni shauri la uhujumu uchumi namba tatu la mwaka 2022 ambapo kulikua na jumla ya mashahidi 32 kutoka mikoa ya lindi, mtwara, Ruvuma, dar es salaam, Dodoma na morogoro na vielelezo 35.
Kesi hii ilikua chini ya hakimu mkazi mfawidhi consolata singano ambapo upande wa jamuhuri ukiongozwa na wakili wa serikali godfrey mramba ambapo ameiambia mahakama yakwamba watuhumiwa walifanya vitendo vya uzalilishaji wa kingono kwa kuwaingilia wanawake wawilia bila ridhaa yao na kuwasababishia hasara kiuchumi kwa kuwaibia kiasi hicho cha fedha huku upande wa watuhumiwa wakiongozwa na wakili hagai mwambingu wakikana makossa yote 16.
Hukumu hii imesomwa ndani ya saa nne na dakika 40 ambapo baada ya kusikiliza pande zote mili ndipo hakimu akatoa hukumu kwenda jela kila mmoja miaka 30 kwa kosa la kubaka.
Makossa manne yaan la 3,4,5,6,7 la wizi kila kosa kutumikia kifungo cha miaka mitano kila mmoja.
Kuhusu kosa la nane la mtuhumiwa jonh mkondo kughushi nyaraka za benki yeye amehukumiwa kwenda jela miaka saba na kosa la tisa la kufoji nyaraka kwa wote waili nalo wataenda jela miaka saba kila mmoja.
Aidha kosa la kumi la kutoa nyaraka za uongo wote wawili watatumikia kifungo cha miaka saba kila mmoja na kosa la 12,13 na 14 kwa mshatakiwa wa kwanza kazili kaftani kusajili laini za simu kwa kutumia majina ya watu na kuzitumia bila ridhaa yao kinyume na sharia ya mawasliano na posta atatumikia kifungo cha miezi 36 jela au kulipa faini ya shilingi milioni 15.
Kosa la 15 la utakatishaji fedha kwa mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka 20 na huku kosa la 16 pia la utakatishaji fedha wote wawili watatumikia pia kifungo cha miaka 20 jela.
Bada ya kuwahukumu kisha hakimu singano akasema mtuhumiwa wa kwanza kazili atatakiwa kumlipa fidia muhanga wa ubakaji shilingi milioni 5 na kosa la tatu kwa mshatkiwa wa pili nae atalipa fidia kwa muhanga wa kubakwa shilingi milioni 5.
No comments:
Post a Comment