MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI UGANDA-TANZANIA WAFIKIA ASILIMIA 29.
Na Al odia Babara, Bukoba Mradi wa bomba la mafuta ghafi unaotekelezwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania umefikia asilimia 29. Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya sh.trilioni 8 ulisainiwa mkataba wake mwaka 2021 kati ya Rais wa Uganda Yowel Kaguta Museven pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi unaendelea kutekelezwa na umefikia asilimia 29. Afisa katika kitengo cha mawasiliano bomba la mafuta EACOP Abass Abraham akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Kagera June 03, mwaka huu juu ya mwongozo kuhusu mradi wa bomba hilo amesema kuwa, hadi sasa mabomba yaliyopokelewa ni ya kusambaza umbali wa kilomita 500 na kituo cha kupokea mabomba na kuyaboresha kiko mkoa wa Tabora. "Asilimia 80 ya bomba la mafuta ziko nchini Tanzania na asilimia 20 ziko upande wa Uganda, kwa Uganda ni kilomita 296 na upande wa Tanzania ni kilomita 1,147 bomba litapita katika wilaya nane"amesema Abraham Abraham am...