Waziri wa Nishati ambaye
pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya
utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za
Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi
kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa
REA awamu ya tatu.
...............................................
Waziri wa Nishati,Dkt
Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City International ambaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati
alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato.

Ambapo Diwani wa kata ya
Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa
nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.

Mmoja kati ya
wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara zao.

Aidha kutokana na maombi
hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi
Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo
kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.

“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi wa usambazaji wa
umeme vijijini Mkoani
Geita,unatekelezwa na mkandarasi wa Shirika la White City
International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi 16 kwenye
jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani humo na jumla ya fedha ambazo
zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni Sh Bilioni 78.56.

No comments:
Post a Comment