Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, (kulia) mwenye kofia pembeni yake ni Diwani viti maalum Magomeni, Shumina Rashidi wakizindua kisima cha maji shule ya msingi Kerege wilayani Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, akiwa na viongozi waandaamizi wa jumuiya hiyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji kilichochimbwa Shule ya Msingi Kerege.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima kilichochimbwa kwa msaada wa jumuiya ya watu wa korea kusini katika shule ya msingi Kerege.
.............................................
Jumuiya
ya watu wa korea kusini
waishio Tanzania
na Afrika kwa ujumla wametoa msaada wa visima katika shule za msingi Kerege na
Mapinga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, mam Lee Hae Meng ambae
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema wamefikia uamuzi huo ili
kusaidia maeneo yenye shida ya maji hasa katika maeneo ya shule.
Alisema
wameguswa na mazingira ya shule msingi Kerege na hivyo kuamua kujitolea katika
kusaidia kisima cha maji ili wanafunzi katika shule hiyo waondokane na adha ya
kutafuta maji.
Akisoma
risala mbele ya mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kerege Ester Afia
Awino alisema wanaishukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo wa maji kwani ni
miongoni mwa matatizo yaliyokuwa yanaikabili shule hiyo.
Alisema
pamoja na kupata maji bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo
upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo alisema kwa sasa shule hiyo yenye
wanafunzi 1,129 ina upungufu wa vyumba vya madarasa sita.
Alisema
hali hiyo imetokana na ongezeko la wanafunzi waliojitokeza kuandikishwa shule
katika kipindi hiki ambacho serikali imetangaza Elimu bure.
Akizungumzia
hali ya taaluma ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Msingi, Alex Mwakawago alisema
shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma hivyo kuindolea
changamoto ni kuisaidia katika kuku taaluma.
Alisema
upatikanaji wa maji katika shule hiyo kutaongeza ari kwa wananfunzi na kupata
muda mzuri wa masomo na hatimae kuongeza kiwango cha taaluma.
Nae
Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Saidi Ngatipula lisema anaishukuru jumuiya hiyo ya watu wa korea kusini
kwa msaada wa visima ambapo umepunguza adha ya maji katika eneo la Kerege.
Alisema
Jumuiya hiyo kwa sasa imechimba visima vitatu ndani ya kata ya Kerege ambapo ni
shule ya msingi Kerege, Shule ya Msingi Mapinga na Shule ya Sekondari Kerege.
Aidha,
alisema kuwa, wanathamini msaada huo na kwamba watavitunza visima hivyo ili
waendelee kufaidika navyo kwa sku nyingi zaidi.
Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Saidi Ngatipula, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kisima shule ya msingi Kerege wilayani Bagamoyo.
Kutoka kulia ni Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Saidi Ngatipula, katikati ni Diwani wa viti Maalum Shumina Rashidi na wa kwanza Kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Yombo, Togo Malihega, wakishuhudia uzinduzi wa kisima cha maji shule ya msingi Kerege.
Kaimu Afisa Elimu Msingi, Alex Mwakawago akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima shule ya msingi Kerege.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Juliasi Mwang'anda akimkaribisha mgeni
rasmi.
No comments:
Post a Comment