Diwani
wa kata ya Yombo, Mohamed Usinga akitoa msimamo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri
kuhusu kuiktaa Taarifa ya utekelezaji wa ilani.
............................................
Madiwani
wa Halmashauri ya Bagamoyo wameikataa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya 2017 kufuatia
taarifa hiyo kuwa na mapungufu kadhaa.
Madiwani
hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issah
wameikataa taarifa hiyo mara ilipofika katika utekelezai wa miradi inayohusu
idara ya uvuvi ambapo miradi iliyoainishwa ndani ya taarifa hiyo haipo katika
maeneo husika jambo liliwatia hasira madiwani hao na kuamua kuirudisha Taarifa
yote kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili ifanyiwe marekebisho.
Akitoa
maamuzi ya Baraza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally alisema
wanairudisha taarifa yote ka Mkurugenzi ili ipitiwe upya na kunyiwa marekebisho
katika maeneo ambayo madiwani hawakuridhika nayo.
Kabla
ya Mwenyekiti wa Halmashauri kutoa msimamo huo wa Baraza, madiwani hao walisema
ifike wakati sasa wataalamu wa Halmashauri wafanye kazi kwa kuzingatia sheria
na kanuni za kazi ili kila mmoja achunge mipaka yake.
Walisema
katika kikao cha Baraza kuleta tarifa inayokwenda kinyume na uhalisia katika
utekelezaji wa miradi ni kukiuka sheria, na kwamba baraza halitasita kumuwajibisha
mtumishi yeyote anaekiuka sheriaa kwa kushindwa kutoa taarifa sahihi za
utekelezaji wa ilani.
Walisema
madiwani ni viongozi wanaochaguliwa na wananchi kwa lengo la kusimmamia
utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa manufaa ya wananchi hivyo si vyema
wataalamu wa Halmashauri wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ni wazi
kuwa wanawatengezea mazingira magumu madiwani ambao watarudi kwa wananchi
kuomba kura kwaajili ya kurudi tena madarakani.
Aidha,
Madiwani hao waliwataka wataalamu wa Halmashauri wanapofika katika utekelezaji
wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali wawasiliane na viongozi wa kata
husika ili kuleta ushirikiano kati ya wataalamu hao na viongozi wa kata
wakiwemo watendai wa kata na madiwani ili kuondoa sintofahamu inayoweza
kujitokeza siku ya kuwasilisha taarifa.
Katika
taarifa hiyo idara ya uvui imetaja kujenga kwa mabwawa ya samaki katika baadhi
ya maeneo huku madiwani wakishangaa kwakuwa hawajawahi kuyaona mabwawa hayo
kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu amekiri kupokea taarifa hiyo na kwenda kuifanyia marekebisho na wataalamu wake ili baadae iwasilishwe ikiwa imekamilika.
Wakati
huohuo Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Salum kamote amewaonya wakuu wa idara
ambao wanatabia ya kutoa taarifa zisizo sahihi kwani kwa kufanya hivyo
wanachangia kuidhoofisha chama tawala katika mikakati yake ya kusimamia
utekelezaji wa ilani uchaguzi jambo linaidhoofisha serikali iliyopo madarakani
kwa ujumla.
Alisema
ni vyema taarifa ikawa wazi kama kuna mradi
haujatekelezwa ili chama kijue wapi kwenye madhaifu ili nguvu zielekezwe hapo
na kuhkikisha miradi hiyo inateekelezwa kuliko kutoa taarifa za uongo.
Aidha,
katibu huyo wa CCM wilaya ya Bagamoyo amewapongeza madiwani Halmashauri ya
Bagamoyo kwa uwasilishaji mzuri wa taarifa za kata na hatua waliyochukua
kuikataa taarifa ya utekelezaji wa ilani.
Alisema
Madiwani ndio wasimamizi wa miradi hivyo wanapaswa kuwa imara katika
kuhakikisha miradi yote iliyopangwa na kutengewa mafungu inatekelezwa kwa
ukamilifu wake ili kujenga imani kwa wananchi ambao ndio walipewa ahadi za
kutekeleza mambo mbalimbali.
Kikao
hicho cha Baraza la madiwani Halmashuri ya Bagamoyo kimeanza leo jumatano
February 14 ambapo kimejadili taarifa za robo ya pili ambapo madiwani waliweza
kuwasilisha taarifa za kata zao.
Madiwani
wa Halmashauri ya Bagamoyo wakifuatilia kwa karibu uwasilishwaji wa taarifa za kata pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ambayo baadae waliikataa kwa pamoja na kumrudishia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Latu kwaajili ya Marekebisho.
Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo wakifuatilia kwa karibu
uwasilishwaji wa taarifa za kata pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ambayo baadae waliikataa kwa pamoja na kumrudishia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Fatuma Latu kwaajili ya Marekebisho.
No comments:
Post a Comment