Naibu
waziri wa nishati awasha umeme kituo cha Mbagala baada ya mradi huo kukamilika.
Kufuatia
kuwashwa kwa kituo hicho, Wananchi wa Mbagala ,Kigamboni
,Tandika na Mkuranga na Wenye Viwanda watapata Umeme wenye Nguvu na wenye
uhakika ambao hautokatika.
Naibu
waziri wa Nishati, amewapongeza wananchi wakazi wa maeneo hayo Kwa kuwa na
subira huku akiwapa pole kwa kero ya umeme ya muda Mrefu.
Aidha,
alisema amewashukuru Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Kigamboni Dk Ndungulile
na Mhe Mangungu na Wakuu wa Wilaya Kwa kufuatilia Jitahada za kuondosha Kero hiyo ya Upatikanaji wa Nishati ya Uhakika
katika Maeneo hayo.
Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa
kutekeleza mradi huo ili wananchi waondokane na kero hiyo.
Alisema kufuatia ushirikiano alionao yeye pamoja na
Waziri wa nishati Dk Medard Kalemani wameweza kufanikisha Miradi mbalimbali ya
Nishati ya umeme hapa nchini hali inayopelekea wananchi kujenga imani na
serikali yao ya
awamu ya tano katika utekelezaji wa miradi.
Aliongeza kwa kusema kuwa, kufuatia ushirikiano na
Waziri wa nishati, imepelekea kuwa karibu na Wataalam wote wa TANESCO pamoja na
Wakandarasi na hatimae kufanikisha mradi huo na miradi mingine iliyo chini ya wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment