WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9 kuboresha
vituo vya afya 170 nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya ya Mama na Mtoto
kwa lengo la kuokoa maisha yao.
Amsema
Serikali itaendelea kukarabati na kupanua miundombinu ya kutolea huduma pamoja
na kununua vifaa vya kisasa katika Hospitali za Mloganzila, Benjamini Mkapa, Dodoma na Hosptali za
Rufaa katika Mikoa na Kanda.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) wakati akizindua
jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Amana
iliyopo wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Jengo
hilo la ghorofa
mbili limejengwa kwa ufadhili wa kundi la kampuni za AMSONS na lina thamani ya
sh bilioni 1.2.
Amesema uzinduzi
wa jengo hilo
unakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt. John Magufuli za kuimarisha sekta
ya afya na kuifanya kuwa miongoni mwa sekta za kipaumbele.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi.
“Mfano, Hospitali za Rufaa za Amana, Mwananyamala na Temeke, zimeendelea
kuhudumia wagonjwa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya vya Serikali, binafsi
na vya dini kutoka mikoa jirani ya Pwani, Morogoro na Lindi.
Pia
amesema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, kuhusu kuwapatia wananchi huduma bora za
afya pamoja na kujenga hospitali nyingine za Rufaa kwa ajili ya Kanda ya
Kusini, Kati na Magharibi.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ya idadi ndogo ya watumishi na ukosefu wa huduma za uangalizi
maalumu (ICU) katika hospital ya Amana, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea
kufanyia kazi changamoto zote zilizopo katika sekta ya afya zikiwemo n aza
hospital hiyo.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wadau
mbalimbali pamoja na kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa huduma
za afya nchini zinaboreshwa.
Hivyo,
alitumia fursa hiyo na kulipongeza kundi la kampuni za AMSON’s lililoamua
kujenga jengo la mama na mtoto katika hospital hiyo kwa ushawishi wa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda.
Awali, Mganga
Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana, Dkt. Meshack Shimwella
alisema wazazi wanaolazwa katika hospitali hiyo kwa siku ni 180 hadi 250 na
uwezo wa hospitali ni vitanda 353, ambapo vitanda 250 vinatumika wodi ya
wazazi.
Alisema
idadi hiyo hailingani na idadi ya wagonjwa, hivyo kusababisha wakati mwingine
wagonjwa kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kutokana na kasi ya
ongezeko wa wagonjwa wanaolazwa hususani wodi ya watoto na akinamama.
Dkt.
Shimwella alisema wamefanikiwa kuongeza jingo la kutolea huduma ya mama na
mtoto lenye ghorofa mbili ilililojengwa kwa ufadhili wa AMSONS lenye uwezo wa
vitanda 100, ambalo ndilo liliongeza idadi ya vitanda kutoka 253 hadi kufikia
353.
“Kutokana
kukamilika kwa jengo hilo kwa sasa akinamama wanaonyonyesha wanalala wakiwa
mmoja mmoja, watoto wachanga wanahudumiwa katika mazingira mazuri yanayofanana
na viwango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Makonda aliwashukuru
wafadhili waliojenga jengo hilo kwa sababu si kila mtu anayekwenda hospitali na
kukuta changamoto na akaamua kuzifanyia kazi.
Bw.
Makonda alisema awali akinamama walikuwa wanalala hadi watatu katika kitanda
kimoja, hivyo madhumuni ya ujenzi wa jego hilo ni kupunguza msongamano katika
wodi ya wazazi.
No comments:
Post a Comment