MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo,(kulia)akielekeza jambo baada ya kuonyeshwa ramani ya
ghala la korosho ambapo linatarajia kujengwa huko Mkuranga,
wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa ghala hilo .
.............................................
Na
Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
MKUU
wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza bodi ya Korosho Tanzania
(CBT) kuhakikisha inamlipa ,malipo ya awali kiasi cha sh.bilioni 1.6,
mkandarasi wa ghala la kuhifadhia korosho wilayani Mkuranga.
Alitoa
agizo hilo ,wilayani Mkuranga alipotembelea
ujenzi wa ghala hilo
linalojengwa na kampuni ya BQ Contractors Ltd .
Alieleza
kabla ya ujenzi waliingia mkataba wa kulipa asilimia 30 ya malipo ya awali ya
ujenzi wa ghala hilo
la kisasa ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.5 hadi kukamilika
kwake.
Aidha
Ndikilo alisema, kampuni hiyo ilitoa malalamiko kuwa zimepita siku 52 wakiwa
hawajapewa hata shilingi moja kwa ajili ya ujenzi huo hali ambayo inasababisha
ujenzi huo kuwa mashakani kukamilika kwa wakati.
“CBT
ihakikishe inatoa fedha hizo ndani ya wiki hii, bodi ya korosho ambao ndiyo
wamiliki wa ghala hilo
na endapo watashindwa kufanya hivyo atawapeleka kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya
hatua zaidi”;
“Mkurugenzi
wa bodi hiyo itabidi wakutane Dodoma
kwa ajili ya kueleza ni sababu gani inawafanya washindwe kumlipa mkandarasi
huyo,” alisema Ndikilo.
Alisema
serikali kwa kushirikiana na bodi ya korosho walikubaliana kujenga ghala hilo ili kuwe na ghala
moja kwa kila wilaya tatu za Mkuranga, Kibaha na Rufiji ambako ndiko zinalimwa
korosho nyingi.
Ndikilo
alieleza lengo la kuwa na ghala la uhakika ni kufanikisha mfumo wa
stakabadhi ghalani.
“Kuanzia
msimu ujao korosho zote zitauzwa kwenye ghala moja kubwa badala ya kutumia
maghala ya watu binafsi ama ya vyama vya msingi vya ushirika ambao wanaonekana
kufanya hujuma kwa kuweka korosho ambazo hazina viwango ,:;ambapo kwa msimu huu
tatizo lilikuwa kubwa sana,”
alifafanua Ndikilo.
Hata
hivyo ,alieleza kutotolewa fedha hizo kutasababisha ujenzi huo kutokamilika kwa
wakati kutokana na hali ya mvua za masika unaokuja ambazo zitasababisha ujenzi
huo kushindwa kufanyika katika kipindi lengwa.
Nae
mwakilishi wa bodi ya korosho Japhari Matata alikiri kucheleweshwa kwa fedha
hizo .
Alisema
kwasasa taratibu za kuzipata fedha hizo zinaendelea ili kumpatia mkandarasi
huyo.
Matata
alisema atalifikisha suala hilo kwa wahusika kwa ajili ya
kuhakikisha linafanikiwa ili ujenzi huo ukamilike mwezi wa
nane kipindi ambacho ndicho ilipangwa ukamilike.
Awali
akitoa taarifa kuhusu ujenzi huo, meneja wa maendeleo ya biashara wa kampuni
hiyo Hilu Bura, alisema changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya
ujenzi huo ambao ulianza Oktoba mwaka jana.
Alitaja
changamoto nyingine ni eneo hilo kuwa na maji kwa wingi hivyo endapo fedha
zitachelewa kutasababisha kujenga kipindi cha mvua za masika ambacho
kinakaribia kuanza.
Bura
alimuomba mkuu wa mkoa huyo wa Pwani kuwasaidia ili waweze kupatiwa fedha za
awali.
No comments:
Post a Comment