WAZIRI
wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akikagua pikipiki ambazo
zimeshikiliwakatika kituo cha polisi pangani. ameagiza polisi nchini kuziachia
pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na
wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
…………………………………………
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini
kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo
waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
Dk Mwigulu amesema yale
yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale
wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza
na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu
wamekosea wapi.
“Wapeni masomo wamekosea wapi
walekezeni na waliowabishi waelekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma
chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunawo, tutumie huu mkono wakutatua
kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu
Alisema kuwa ipo haja ya vijana
sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali
ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani
kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
No comments:
Post a Comment