WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu
(CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI).
Akiwa hospitalini hapo leo
(Jumamosi, Februari 10, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta
Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa
vizuri.
Pia
Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti pacha walioungana Consolata na
Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI).
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba Serikali
inadhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari
wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea
katika shughuli zao za kila siku
Kwa
upande wake, Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na
kwenda kumjulia hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa
huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.
Kwa
upande wao Maria na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za matibabu
wanazozipata na kwa sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa
kwenda kuwajulia hali na kumtakia kheri katika shughuli zake
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI,
FEBRUARI 10, 2018.
No comments:
Post a Comment