Diwani
wa viti Maalum Tarafa ya Yombo,
Togo Malihega
(kulia) akiongoza kina mama wa UWT kata ya Kerege walipotembelea ujenzi wa
kituo cha Afya Kerege, leo Tarehe 01 February 2018.
...........................................................
Umoja
wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kata ya Kerege Wilayani Bagamoyo wametembelea
kituo cha Afya Kerege kujionea ujenzi wa kituo hicho.
Umoja
huo wa Wanawake wa Tanzania
katika kutembelea kituo hicho wamepata nafasi ya kufanya usafi katika kituo
hicho ambacho kinaendelea na ujenzi kwa sasa.
Aidha,
walisema wanamipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kutenga
fedha kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya mbacho awali ilikuwa ni
Zahanati.
Walisema
ujenzi wa kituo hicho cha Afya utasaidia kinamama wa kata ya Kerege na maeneo
ya jirani kupata huduma ya uzazi karibu ukilinganisha na sasa ambapo hulazimika
kufika Hospitali ya wilaya kwaajili ya huduma hiyo.
Walisema
kwa muda mrefu wananchi wa Kerege na maeneo ya jirani wamekuwa wakipata tabu kujifungua
huku wengine wakipoteza maisha kutokana na umbali wa kufuata huduma ya uzazi.
Waliongeza
kwa kusema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha Afya kata ya Kerege ni kielelezo
tosha cha kuona Serikali ya chama cha Mapinduzi inasimamia ilani yake hali
inayopelekea kuweza kutekeleza miradi
mbali.
Walisema
kufuatia Ujenzi huo ni wazi kuwa wananchi wataendelea kujenga imani na Chama
Cha Mapinduzi na Serikali yake kutokana na utekelezaji wa ahadi zake kwao.
Mtaalamu
wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mhandisi wa wilaya, Sikutegemea Daudi alisema majengo
hayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika na kwamba hivi karibuni majengo
hayo yatakabidhiwa ili yaanze kazi.
Ujenzi
wa kituo cha Afya Kerege ni mpango wa serikali katika kuhakikisha inaongeza
vituo vya Afya nchini ambapo kata hiyo ni miongoni mwa kata zilizopata fedha za
ujenzi huo.
Majengo
yaliyojengwa mpaka sasa ni jengo la wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, Maabara
na jengo watumishi.
Kufuatia
kugawanywa kwa Halmashauri ya Bagamoyo na kupatikana Halmashauri ya Chalinze,
Halmashauri ya Bagamoyo imebaki bila ya kituo cha Afya.
Kukamilika
kwa kituo cha Afya Kerege kutaifanya Halmashauri ya Bagamoyo kuwa na Kituo
kimoja cha Afya kati ya kata 11.
Kina mama wa UWT kata ya Kerege wakiingia ndani ya jengo la upasuaji walipotembelea ujenzi wa
kituo cha Afya Kerege leo Tarehe 01 February 2018.
Kina mama wa UWT kata ya Kerege wakishangilia mara baada ya kuingia ndani ya jengo la upasuaji walipotembelea ujenzi wa
kituo cha Afya Kerege leo Tarehe 01 February 2018.
Muonekano
wa majengo ya kituo cha Afya Kerege wilayani Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment