Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi anayejenga daraja wa Kimalamisale wilayani
Kisarawe kufanyakazi usiku na mchana ili daraja hilo liweze kukamilika kabla ya Mvua za
masika hazijaanza.
Waziri
Jafo ametoa agizo hilo alipotembelea kukagua
mradi wa ujenzi wa daraja hilo
ambao unagharimu kiasi cha Sh.Milioni 390.
Hatua
hiyo ya Jafo imetokana na mradi huo kuchelewa hapo awali kutokana na Mvua kubwa
za vuli zilizokuwa zinanyesha.
Amesema
mradi huo unatarajiwa kuwa kiungo muafaka kwa barabara ya Kimalamisale ambapo
kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi.
Amebainisha
kuwa kwasasa mvua zinaponyesha magari yanashindwa kupita kutokana kujaa maji
mengi katika mto Muyombo unaotenganisha wilaya ya Kibaha na Kisarawe mkoani
Pwani.
Katika
ukaguzi huo, Mkandarasi wa mradi huo amemwambia Waziri Jafo kuwa ameshanunua
jenerata kubwa ambalo watalitumia wakati wa usiku ili aweze kukamilisha ujenzi
huo.
Ameahidi
kwamba watajitahidi kufanyakazi kwa kasi kubwa ili kuwahi Mvua za masika
na wasipate hasara ya kuchelewesha mradi.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
No comments:
Post a Comment