Waziri wa Elimu na Mafunzo
Profesa Joyce Ndalichako na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Injinia Hamad Yusuph
Masauni wakimfariji mama mzazi wa marehemu Akwiline Baftaha Mwanafunzi wa Cho
cha Usafirishaji NIT aliyefariki kwa majeraha baada ya kujeruhiwa
na risasi juzi.
Akiwa kwenye daladala. Kufuatia vurugu za maanamano ya
wafuasi wa Chadema ,Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli ametuma salami za rambirambi kwa familia kufuatia kifo hicho.
....................................
Serikali
imewahakikishia Watanzania kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya
uchunguzi kufuatia kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Akwilina
Baftaha Akwilini, aliyefariki kwa kupigwa risasi mwishoni mwa wiki iliyopita
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema kuwa Serikali itahakikisha
uchunguzi huo unafanyika kwa weledi na utaalamu ili haki iweze kupatikana na
yeyote aliyehusika atachukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
“Nawasihi
watanzania kuwa na subira ili uchunguzi ufanyike na tutahakikisha uchunguzi huo
unafanyika haraka iwezekanavyo na baada ya kukamilika wote waliohusika
watachukuliwa hatua za kisheria”, alisisitiza Masauni.
Kwa
upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako alisema
kuwa Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanafunzi
huyo ambacho kilitokea wakati wa kudhibiti maandamano yaliyokuwa yakifanyika
katika eneo la Mkwajuni, wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
“Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha
mwanafunzi Akwilina na anaungana na wazazi, familia, ndugu, jamaa na watanzania
wote kuwapa pole za dhati kutokana na msiba huo”, alisema Ndalichako.
Aidha
Ndalichako alibainisha kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itagharamia
shughuli zote za mazishi ya mwanafunzi huyo na amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara
hiyo kusimamia shughuli zote za msiba huo.
Pia Ndalichako
alitoa rai kwa watanzania kujiepusha na vitendo vyote ambavyo vinaweza
kusababisha maafa kwa watu wasio na hatia.
No comments:
Post a Comment