Meneja wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro
(wa nne kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga (mwenye suti) moja ya vifaatiba walivyotoa msaada kwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, wanaoshuhudia wa pili kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya bagamoyo, Ally Ally Issa na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Hospitali ya Wilaya Bagamoyo, Mwajuma Saidi Masaiganah.
...............................................
Benki
ya NMB imesaidia vifaa tiba katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo vyenye
thamani ya shilingi milioni tano.
Akizungumza
katika kukabidhi vifa hivyo, Meneja wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro
alisema Benki hiyo imefikia hatua hiyo ikiwa ni katika mipango yake ya
kurudisha faida inayopata kwenye jamii.
Alisema
NMB katika mipango yake imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za
kijamii kama vile kusaidia katika sekta ya Elimu, kusaidia vifaa vya ujenzi,
sekta ya Afya na kusaidia watu katika kipindi cha majanga kama
ya mafuriko na ajali mbalimbali.
Alisema
Hospitali ni sehemu ambayo kila mwana jamii anafika kupata huduma za matibabu
na hivyo kupeleka msada katika hospitali ni sawa na kusaidia jamii nzima.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, Benki ya NMB ni Benki pekee yenye matawi mengi nchini na hivyo
kuwa na wateja wengi hali inayopelekea kufikiria kuridisha fadhila kwa jamii
ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
Akipokea
msaada huo, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga ameishukuru Benki hiyo kwa
msaada huo na kusema kuwa ni kuonyesha mahusiano mema baina ya Benki hiyo na
Serikali.
Alisema
vifa hivyo vitasaidia kwa Hospitali ya Bagamoyo kwakuwa Hospitali hiyo
inahudumia watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Bagamoyo.
Wakati
huohuo, Mkuu huyo wa wilaya huyo
amewataka madiwani katika halmashauri ya Bagamoyo kuandaa maeneo kwenye kata
zao ya kujenga zahanati ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali
ya wilaya.
Alisema
kuwepo kwa Zahanati kwenye kata kutasaidia wagonjwa kutibiwa kwenye kata zao na
kwamba watakaokwenda Hospitali ya wilaya ni wale ambao wameshindikana kutibiwa
kwenye zahanati.
Nae
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Salvio Wikesi alisema anatoa
shukrani kwa Benki ya NMB kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitasaidi katika
kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika Hospitali hiyo.
Alisema
katika vifaa vilivyotolewa ni pamoja Delivery kit moja ambapo alisema kwenye
muongozo wa wizara ya afya Hospitali ya Bagamoyo inatakiwa kuwa na Delivery kit
10 na kwamba hospitali hiyo sasa ina Delivery kit tano baada ya kupokea moja
kutoka NMB.
Vifaa
hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni tano vilivyotolewa na benki ya NMB ni
pamoja na Mashuka 35, Vitanda 6 pamoa na
magodoro yake, Kitanda cha kuifungulia 1, Seti 1 ya vifaa vya kujifungulia (Delivery
kit) na Mashine ya kupimia BP 1.
Meneja
wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro
(wa tano kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga
(wa tatu kushoto) moja ya vifaatiba walivyotoa msaada kwa Hospitali ya
Wilaya ya Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo, Mwajuma Saidi Masiganah ( wa tatu kushoto, kwa pamoja wakimkabidhi kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Dkt. Salvio Wikesi (katikati) wa tatu kulia ni Meneja wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro, Meneja wa NMB tawi la Bagamoyo wakishuhudia baada ya wao kukabidhi kwa Mkuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, akitoa neno la shukrani kwa NMB mara baada ya kupokea msaada wa vifaatiba.
Meneja
wa NMB kanda ya Mashariki, Aikasia Muro, akizungumza wakati wa kukabidhi vifaatiba hivyo katika ukumbi wa Halmashauri Bagamoyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Salvio Wikesi, akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa kutafuta wafadhili pamoja NMB kukubali kusaidia vifaatiba katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Timu ya wasimamizi wa Afya Halmashauri ya Bagamoyo (CHMT) wakifuatilia kwa karibu makabidhiano ya vifaatiba kutoka kwa Benki ya NMB yayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Bagamoyo.
Meneja wa NMB tawi la Bagamoyo (kulia) akifuatilia makabidhiano ya vifaatiba vyenye thamani ya shilingi milioni 5, vilivyotolewa na Benki hiyo kwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Timu ya kutoka NMB tawi la Bagamoyo wakiongozwa na Meneja wa kanda ya Mashariki, Aikasia Muro, (wa pili kulia) wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, (wa pili kushoto) wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Afya, Mwajuma Saidi Masaigana, na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally.
Timu ya wasimamizi wa Afya Halmashauri ya Bagamoyo (CHMT) wakipiga picha ya pamoja na meza kuu.

No comments:
Post a Comment