MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM)wilayani Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ,akizungumza na wanachama wa chama
hicho na baadhi ya wananchi (hawapo pichani) huko kata ya Miono wilaya Bagamoyo.
......................................
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo,alhaj Abdul Sharifu amefuta
waraka uliotolewa wilayani hapo, ambao unakataza viongozi wa chama kutokuwa na
fursa ya kuwahoji watendaji wa serikali.
Aliyasema
hayo baada ya kufanyika sherehe za miaka 41 ya CCM katika kata za Mbwewe, Miono
na Lugoba .
Alhaj
Sharifu alisema waraka huo unasababisha baadhi ya watendaji kutowajibika
ipasavyo kwa wananchi.
Alielezea
waraka huo unaonekana una maslahi ya watu binafsi ambao unakwenda kinyume na
maslahi ya wananchi hivyo hauna manufaa yoyote zaidi ya kuwakandamiza wananchi.
“Naufuta
maana haiwezekani watendaji wa serikali waachwe wafanye wanavyotaka hata
wakiharibu tusiwahoji ,wakati chama kina wajibu wa watendaji wa serikali ,”
alisema Sharifu.
Aidha
Sharifu alisema,baadhi ya mambo yamekuwa hayaendi kutokana na watendaji hao
kujisahau na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwani hakuna watu wa kuwahoji.
“Kila
siku Rais anasisitiza chama ndiyo kimeunda serikali hivyo watendaji wake lazima
wasimamiwe na chama ,hatuwezi kuona mambo yanaharibika halafu tukae kimya
ikifika nyakati za uchaguzi tunaonekana hatujafanya lolote,Hili halikubaliki,”
alisema Sharifu.
Alisema
ilani inayotekelezwa ni ya CCM hivyo lazima viongozi wa CCM wasimamie watendaji
na hata ikiwezekana kuwaondoa wale ambao wanashindwa kuwajibika kwenye nafasi
zao.
Nae
mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Abubakary Mlawa alisema wamejipanga vizuri
kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inakamilika kwa muda
uliopangwa.
Mlawa
alisema kuwa jumuiya zote za chama zimeungana kuhakikisha zinawatumikia
wananchi kwa kuhamasisha masuala ya maendeleo na kuibua miradi ya maendeleo
ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji, barabara, kilimo na mifugo.
No comments:
Post a Comment