Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki matembezi ya mahafali
ya 34 ya Chuko Kikuu Huria pamoja na Mkuu wa chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu
Mizengo Pinda (kulia) kuelekea kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi kwenye
sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.
..............................................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewakumbusha wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwa Vyeti walivyotunukiwa
ni tuzo halali kwa juhudi na jitihada walizoonesha darasani.
Makamu
wa Rais aliyasema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria
yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri Bariadi mkoani Simiyu.
Makamu
wa Rais alisema “ Jamii inategemea mtaipatia tuzo ya utendaji bora na ufanisi
katika fani zenu utakao akisi viwango vilivyoainishwa kwenye vyeti vyenu”.
Makamu
wa Rais aliupongeza uongozi wa chuo kwa jitihada zake katika kutekeleza
maelekezo ya Mhe. Rais hasa katika sula la Uchumi wa Viwanda ambapo chuo hicho
kimefanya Kongamano kubwa la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda mjini Bariadi lakini
pia chuo hicho kipo kwenye mchakato wa Kigoda cha kiprofesa cha Viwanda na
Maendeleo.
Makamu
wa Rais aliwakumbusha uongozi wa chuo katika jitihada zake za kutekeleza
majukumu ya chuo , uendelee kujikita kwenye kauli mbiu yake Elimu Bora na Nafuu
kwa Wote .
Katika
Mahafali hayo ambayo zaidi ya wanafunzi 941 wamehitimu kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara na Zanzibar
pamoja na nchi za jirani ambapo wanafunzi saba (7) walihitimu Shahada ya
Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu Huria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa
mahafali ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi
mkoani Simiyu.
Sehemu
ya Wanafunzi waliohitimu katika Chuo Kikuu Huria wakiwa kwenye sherehe za
mahafali ya 34 ya chuo hicho.
Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment