Posts

BASUTA YATOA TAMKO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Image
  Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) Sheikh Ally Zubeir. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, akiongea kwenye Mkutano huo ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. ............................... Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) limetoa tamko kuelekea uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu 2025. Tamko hilo la BASUTA limetolewa katika Mkutano wake Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Juliasi Nyerere jijini Dar es salaam siku ya tarehe 11 Oktoba 2025.

KAMBAYA ATAHADHARISHA SIASA ZA FUJO

Image
  Na Rashid Mtagaluka, Dar es Salaam Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kada maarufu wa chama hicho, Abdul Kambaya, amewatahadharisha Watanzania na wanasiasa wa upinzani wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa siasa ni mashindano ya hoja, siyo matusi wala fujo. Kambaya alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Makurumla, manispaa ya Ubungo, ambapo aliwataka wananchi kuwa makini na viongozi wanaopotosha jamii kupitia mitandao. “Siasa sio kushindanisha ukubwa wa sauti, hapana. Siasa ni kushindana kwa hoja. Kama wenzetu wana hoja, basi wazilete mezani, siyo kukaa mitandaoni na kuhamasisha watu kufanya maandamano wakati wao wenyewe hawaonekani na hatujui kama bado wako hai au la,” alisema Kambaya huku akishangiliwa na umati wa wananchi. Kambaya aliongeza kuwa baadhi ya watu wanaomchukia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hawafanyi...

KIKWETE ASHIRIKI MAPOKEZI TUZO YA SHUKRANI KWA DKT. SAMIA.

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameshiriki mapokezo ya Tuzo ya Shukrani kwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa alizozifanya akiongoza mapambano kuwatetea na kuwahudumia Watu wenye Ulemavu , zilizopokelewa na Ndg. Kassim Majaliwa Majaliwa , Waziri Mkuu wa JMT kwa niaba yake Jana tarehe 11 Oktoba Dar- Es Salaam.  Tuzo hii ambayo inabeba mrejesho wa shukrani kwa kazi nzuri ambayo Mheshimiwa Rais. Dkt Samia ameifanya kwa watu wenye Ulemavu katika kipindi cha miaka yake minne ya uongozi wake, ni alama ya shukrani toka kwa watu wenye Ulemavu. Kwa upande wake waziri Kikwete, ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mh. Rais kwa jinsi anavyoleta heshima kwenye nchi  na  matunda yake yanaonekana. Naye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa, amewashukuru watu wenye ulemavu kwa kutambua mchango huo wa Mh. Rais na kuwapa salamu pia za Mh. Rais...

DC BAGAMOYO, AWATAKA WANANCHI WAMILIKI ARDHI KISHERIA KUEPUKA UTAPELI.

Image
  MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, amewataka wananchi kurasimisha ardhi ili wapate umiliki kisheria waepukane na utapeli na migogoro ya ardhi. Ndemanga ameyasema hayo Chalinze wakati akizindua Mradi wa Kuboresha Usalama wa Miliki za Ardhi katika Halmashauri ya Chalinze. Amesema kuwa mfumo wa hati za kisasa hauwezeshi mtu kutumia ujanja ujanja kupata hati na kumiliki ardhi kinyume cha utaratibu hivyo kupunguza utapeli na migogoro ya ardhi ambayo ilikithiri. Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Pwani Rugambwa Banyikila amesema kuwa hadi sasa jumla ya wananchi 515 wamekwisha hudumiwa kupitia kliniki ya ardhi ya wiki ya huduma kwa wateja.  Banyikila amesema kuwa zoezi la kliniki ya ardhi kwa wananchi wa wilaya ya chalinze lilianza tarehe Oktoba 7 mwaka huu na linafanyika ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, ambapo limerahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za kisekta kwa wananchi katika maeneo yao. Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya ...

SERIKALI YAHIMIZA TAASISI ZA KULEA YATIMA KULINDA IMANI YA WAHISANI

Image
  Na Albert Kawogo, Bagamoyo  SERIKALI imezitaka taasisi zinazosimamia malezi ya watoto yatima na wale wanaoshi katika mazingira magumu kusimamia miongozo,taratibu na sheria katika matumizi ya misaada mbalimbali wanayopewa ili kujenga imani ya wahisani wanaotoa misaada hiyo     Wito huo umetolewa hivi karibuni  na Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Bagamoyo Abuu Yasin wakati wa sherehe ya miaka 25 ya kuadhimisha kituo cha kuelelea watoto yatima cha Moyo Mmoja kilichoko mjini hapo    Yasin amesema kumekuwa na matatizo ya baadhi ya vituo vya watoto yatima kutumia vibaya misaada ya wahisani hasa fedha jambo ambalo linawakatisha tamaa watoa misaada na madhara yake yanakwenda moja kwa moja kwa walengwa wakuu wa misaada hiyo ambayo ni yatima.    "Sisi kama serikali taratibu na sheria zetu ziko wazi na kazi yetu sisi ni kuwahimiza kufuata miongozo hiyo ili kulinda imani ya wafadhili" Amesema   Aidha Yasin alikisifu kituo cha Moyo Mmoja Trust ku...

MARUFUKU YA WATAWA, MAPADRE KANISA KATOLIKI HAKI AU KIZUIZI ?

Image
  ANAANDIKA  RASHID MTAGALUKA Kauli iliyotolewa Septemba 25, 2025 na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa wa Jimbo Katoliki Lindi, ikiwakataza watawa na waseminari kujihusisha na siasa kwa namna yoyote ile, imeibua mjadala mpana unaohitaji tafakuri ya kina kwa maslahi ya mshikamano wa Taifa letu. Kwa mujibu wa Askofu Pisa, watawa na waseminari hawataruhusiwa hata kufahamika au kutambulishwa kama washiriki wa chama chochote cha kisiasa, wala kuhusishwa na jambo lolote lenye sura ya kisiasa. Kauli hiyo imekuja siku moja tu baada ya Masista wa Ndanda kuonekana wakimuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wake wa kampeni. 1. *Haki* *za* *Kikatiba*  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 20(1), inatamka wazi kuwa: "Kila mtu anao uhuru wa kukusanyika kwa hiari na kushirikiana na watu wengine, na kwa hiari kuanzisha na kushirikiana na vyama na mashirika mengine kwa madhumuni ya kulinda na kuendeleza ma...

WANANCHI WINDE BAGAMOYO, WASHANGAZWA NA KUPANDWA MAWE MAPYA KWENYE ENEO LAO.

Image
  Wananchi wazawa wa eneo la Winde lililopo kitongoji cha Mkwajuni kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo wameshangazwa na uwepo wa mawe yanayoashiria mipaka mipya ndani ya eneo lao. Wakiongea siku ya tarehe 30 Septemba 2025 katika mkutano ulioitishwa na wananchi hao ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu eneo lao wamesema wao ndio wenye eneo hilo na tayari baadhi ya familia wamefuata taratibu za kupima eneo hilo kisheria lakini chakushangaza yanaonekana mawe katika eneo hilo. Mwenyekiti wa Wananchi hao, Muharami Seleman amesema kuwa eneo hilo ni mji wa Kale ambao una historia kubwa hivyo kuna haja ya kuuenzi kwa kuurasimisha na kuweka huduma za kijamii. Seleman amesema kuwa moja ya vitu vya kihistoria ni uwepo wa kaburi lililopo hapo tangu mwaka 1,532 la mtu mweusi, visima vya maji ambayo yanatumika hadi hivi sasa. Amesema kuwa pia eneo hilo maarufu kama namba 56 kuna mji ambao umezama baharini kwani unapakana na bahari, magofu ya kale, vyungu vya kupikia na kuna maeneo kwa ajili y...