Imeelezwa
kuwa wazazi wanapaswa kujiona ni wenye bahati kwa kupata mtoto na kwamba
wanatakiwa kumthamini kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kumpa stahiki zake
zote ikiwemo kumnyonyesha kwa miaka miwili bila kumkatisha.
Akizungumza
katika uzinduzi wa jukwaa la mawasiliano la naweza kupitia smart generation,
Shilole alisema kuna wanawake wengi sana wamekuwa na tabia ya kikatili ya
kumnyima mtoto wake kunyonya kwa muda mrefu, wakihofu usichana wao utakwisha.
Alisema
jambo hilo sio zuri, kupitia jukwaa la naweza atahakikisha anahamasisha wanawake
kuwa na tabia ya kuwathamini watoto wao, waache tabia ya kuwawekea pilipili
katika chuchu mara tu inapofika miezi mitatu.
“Mthamini
mtoto wako, usimkatili mtoto ndani ya miezi mitatu unamnyima ziwa huko ni
kumkosea mtoto, lakini pia ni kujitengenezea mtoto ambaye hana akili, anakuwa
zezeta,” alisema Shilole.
Usiogope
kuwa ziwa litadondoka, ukishakubali kuwa mama huna sababu ya kuwaza kuwa ziwa
lako linadondoka, hakikisha unampa haki zake
Kwa
upande wake balozi Masoud Kipanya, aliwaasa wanaume kuhakikisha mama anasaidiwa
katika kila hatua ya makuzi ya mtoto.
Alisema
ni vizuri wakina baba kuwa mstari wa mbele katika ustawi wa mtoto.
“Baba
bora ni pamoja na kuhakikisha mtoto unamsimamia vya kutosha, idadi ya vifo 30
kwa siku vinavyotokana na uzazi inaweza kupungua kama tutajitahidi kuwa sehemu
makuzi ya mtoto.
Kwa
upande wake mtaalam kutoka taasisi ya 360 fhi Bw. John Bosco akielezea mradi wa
naweza ambao uko ndani ya mradi wa USAID
tulonge afya, alisema naweza ni jukwaa la mawasiliano la kubadilisha tabia,
ni jukwaa ambalo linampa mtanzania uhakika wa afya yake ya kesho, linamuwezesha
baba kuwa baba bora,
Kuwa
baba bora ni pamoja na kuwa karibu wakina mama, kuwahamasisha kwenda kliniki,
kuwasindikiza kwenda katika kituo cha afya, unaweza kuwa baba bora au mama bora
kupitia jukwaa la naweza
Jukwaa
la naweza linaanza safari na mama wakati anapoanza kushika ujauzito,
linamkumbusha mama kwenda kliniki, kutumia chandarua chenye dawa, kutumia
vidonge vinavyomkinga mtoto dhidi ya malaria, kunyonyesha mtoto, kutumia njia
ya afya ya uzazi ili kumkuza mtoto vizuri, linawakumbusha wenzi kuwa na tabia
chanya ya kumlinda mtoto.
Naweza
wanambinu mbalimbali ya kuwafikia jamii, lakini kutokana na ugonjwa wa corona
wamejikita zaidi katika mitandao ya kijamii. Ni jukwaa la mawasiliano kwa lengo
la kubadilisha tabia.
Mabalozi wa jukwaa la naweza,
Kutokana
na umuhimu wa kazi ya jukwaa la naweza viongozi wameamua kuteuwa mabalozi wa
jukwaa hilo ili kufikisha ujumbe mbali zaidi, waliobahatika kuwa mabalozi hao
ni pamoja na msanii maalufu, Shilole na Mtangazaji, Masoud Kipanya.
Siza
“Tumekuwa tukipokea maswali mengi sana kuhusu mradi ambao tumeuzindua wiki
iliyopita, mradi wa kuingiza vitabu nchini Tanzania, vitabu laki moja, ambao
tulisema tulisaini makubaliano na wenzetu kutoka nchini Uingeleza wa kuingiza
vitabu kati ya 20,000 hadi 30,000 kila mwezi
Habari
njema ni kwamba wiki ijayo tunauzindua rasmi mradi huo na vijana wengi
tunategemea wanapata fursa mbalimbali ikiwemo namna ya kushirikiana nao juu ya
kusaidia biashara zao, ambao hawana mitaji ya kutosha,
No comments:
Post a Comment