MBUNGE
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ameweka wazi kuwa vituo vya afya katika
jimbo hilo
vinakabiliwana na ukosefu wa vyumba vya kuhifadhia maiti .
Amesema
changamoto hiyo ni kubwa ambapo husababisha wananchi kupeleka maiti za ndugu
zao kwenye Hospitali teule ya rufaa ya Tumbi na wilaya ya Bagamoyo ambako kuna
mbali mrefu.
Aliyasema
hayo mjini Chalinze,wakati akizungumza na baadhi ya wananchi,na kusema
shida kubwa inatokea hasa pale mgonjwa anapokuwa amefariki.
Ridhiwani
alisema jimbo zima la Chalinze hakuna chumba cha kuhifadhia maiti kwenye vituo
vyote vya afya hali ambayo imekuwa mtihani mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo .
“Hali
ni mbaya kwa wenzetu wa kata ya Kibindu ambao wanapeleka maiti Hospitali ya
Bwagala wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,”
“Wananchi
wanaingia gharama kwenda kuhifadhi maiti sehemu nyingine ambako ni mbali na
maeneo yao”
“Tunaishukuru
serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya pamoja na
zahanati lakini changamoto yetu kubwa ni ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti
ambapo tunajitahidi kufanya njia ili kuhakikisha tunajenga chumba hicho,”
alisema Ridhiwani.
Hata
hivyo, Ridhiwani alisema kata ya Lugoba ambapo kuna kituo cha afya serikali
imetoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kujenga majengo yakiwemo
wodi ya mama na mtoto, maabara, chumba cha kufanyia upasuaji mdogo kwa ajili ya
akinamama na chumba cha kuhifadhia maiti.
Akielezea
suala hilo ,mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema
serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya kwenye zahanati zake 292 na
vituo vya afya 26 ambapo vituo 119 vimekarabatiwa ili kutoa huduma bora.
Alisema
mbali ya hilo
pia inahakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa mkubwa.
Ndikilo
alieleza kwa sasa ni kunahakikishwa kunakuwa na ongezeko kutoka asilimia 73.3
hadi kufikia asilimia 85 hali ambayo amesema inawezekana kutokana na mikakati
iliyowekwa ya upatikanaji wa dawa.
No comments:
Post a Comment