Tuesday, March 20, 2018

VIJANA 20 WAOZESHWA SIKU MOJA MOROGORO.


Taasisi ya The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Sharjah Charity International katika falme za kiarabu UAE pamoja na Mabwana harusi 20 wamefanikiwa kwa pamoja kukamilisha zoezi la ibada ya ndoa ya kiihistoria nchini Tanzania kwa vijana wa kislamu 20.

Ndoa hiyo imefanyika katika makao makuu ya #Taasisi ya the Islamic foundation mjini Morogoro na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka katika mkoa wa Morogoro na maeneo ya jirani huku taasisi ya TIF ikiweza kuratibu shughuli hiyo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza katika Ndoa hiyo ya kihistoria mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE Dkt. Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI ambaye ndiye mgeni Rasmi katika ibada hiyo ya ndoa amewataka vijana kuoa kwa kufuata mafundisho ya Mtume Mohammad (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aaalihi Wa Sallam)

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa TIF itaendelea kusimamia na kudhamini vijana mbalimbali wa kiislamu ili kuweza kufikia malengo yao ya kutekeleza ibada ya ndoa.

Hata hivyo MAMLAKA ya barabara na usafirishaji Dubai RTA Dubai UAE imeikikabidhi kituo cha yatima cha Darul Imaan kinachomilikiwa na taasisi ya The Islamic Foundation Basi la Abiria aina ya Ashok Leyland lenye uwezo wa kubeba abiria 50.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE Dakta Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI katika ziara yake kwa taasisi ya the Islamic foundation mkoani Morogoro na kusema kuwa mamlaka hiyo imeikabidhi kituo hicho ili kuweza kurahisisha huduma za usafiri kwa watoto ya tima wanaolelewa na TIF.

Aidha mamlaka hiyo imekabidhi mabegi 200 kwa watatoto yatima wanaolelewa katika kituo cha taasisi ya the Islamic foundation cha Darul Imaan na kusema kuwa mabegi hayo yatawasaidia watoto hao kwa kiasi kikubwa.

Katika hatua nyingine mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE imetoa baiskeli 25 kwa watoto hao yatima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya the Islamic foundation Aref Nahdi ameishukuru mamlaka hiyo kwa kuona umuhimu wa kuisaidia tif katika kitengo cha Yatima na kusema kuwa tif imefarijika na msaada huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi akizungumza wakati wa hfla hiyo ya kuwaozesha vijana 20 wa kiislamu mjini Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji nchini Dubai UAE, Dakta Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI akizungumza katika hafla hiyo ya kuwaozesha vijana 20 wa kiislamu iliyofanyika Mjini Morogoro nchini Tanzania.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya The Islamic Foundation, Sheikh Ibrahim Twaha (kulia) na Mkurugenzi wa vyombo vya Habari vya Imaan, Ahmed Bawaziri (kushoto) wakiwaongoza vijana 20 wa kiislamu katika zoezi la kuwafungisha ndoa wote kwa siku moja zoezi ambalo limesimamiwa na Taasisi ya 
The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Sharjah Charity International kutoka falme za kiarabu UAE. 
Upande wa chakula mambo yalikuwa hivi.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia ndoa hiyo ya kihistoria hapa nchini.

No comments:

Post a Comment