Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa
Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu
kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi
2019.
...................................
NA
WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine
za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya
nchini.
Hayo
yamezungumzwa jijini Dar es
salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu
kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini.
“Serikali
imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi
bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa
haraka ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri
Ummy.
Aidha
Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua
Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.
Kwa
mujibu wa Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji
kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali
kwa ajili ya msaada wa haraka.
Aidha,
Waziri Ummy alisema kuwa takribani watu laki moja na 60 wana maambukizi
ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba
na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa
ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana
kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal
ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha
Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara
wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki
mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa
kukua na kikohozi cha mara kwa mara.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto
Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa dawa ya
kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni
Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice
Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome Bi. Upendo
Jeremiah.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu
Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es
salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2018.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya
siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2018.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya
wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu
kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe
24 Machi 2018.
No comments:
Post a Comment