Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga
Taraba wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea
mradi wa umeme kijiji cha Negezi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wakati Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea miradi ya umeme.
........................................
Naibu
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amesema Serikali itaendelea na usambazaji
wa nishati ya umeme katika vijiji vyote 50 katika Wilaya ya Kishapu kama ambavyo iliahidi.
Amesema
hayo wilayani humo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
ilipofanya ziara wilaya Kishapu kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kamati
hiyo ikiwa kwenye vijiji vya Negezi na Bulimba ikiambatana pia na uongozi wa
Mkoa na Wilaya, Mhe. Mgalu alisema kuwa mpango wa usambazaji umeme ni wa awamu
na kuwa wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitafikiwa na mradi.
Aliongeza
kuwa vijiji 33 kati ya 50 vitapata umeme wa REA awamu hii ya tatu wakati 17
vitapata nishati hiyo kupitia njia kuu inayounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na
Tabora.
Kwa
upande wake, Kamati hiyo ya Bunge ilisema wataendelea kuikumbusha Serikali
iendelee kutimiza ahadi zake kwa wananchi za kukamilisha miradi ya umeme.
Iliwataka
wananchi ambao wamepitiwa na miradi hii katika vijiji vyao kuichangamkia fursa
na kuomba kuunganishiwa ili kupata huduma hiyo na kujiletea maendeleo.
Aidha
iliwataka wananchi kuboresha aina za makazi yao kadiri ya uwezo wao na kuezeka nyumba zao
kwa bati na kuachana na matembe na hatimaye kuwa na nyumba zilizo bora.
Katika
ziara hiyo kijiji cha Bulimba kilichopo kwenye kata ya Ukenyenge kumezinduliwa
rasmi huduma ya umeme mradi uliokamilshwa kupitia REA na hivyo kutarajiwa
kuwanufaisha wananchi.
Baadhi ya wajumbe Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji
cha Negezi wakati ilipotembelea miradi ya umeme vijijini wilayani Kishapu.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Subira Mgalu (kushoto) akishirikia kucheza ngoma ya Kisukuma akiwa akiwa kijiji
cha Bulimba mabako umeme uliwashwa rasmi baada ya kukamilika usambazaji.
No comments:
Post a Comment