Watu wawili wamekufa wilayani Kasulu mkoani Kigoma
katika ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC
Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi
Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali
hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu
watatu.
Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali
lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo
mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC
Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.
Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya
vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
No comments:
Post a Comment