Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu
zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.
Timu
ambazo zimefuzua hatua ya mtoani ambazo Yanga anaweza kukutana nazo ni Fosa Juniors kutoka Madagascar,CARA
Brazzaville (Con),Costa do Sol ya Msumbiji,Akwa
United na Enyimba za Nigeria,Deportivo Niefanga ya Equatorial Guinea,Welayta Dicha ya Ethiopia,,El
Masry ya Misri,Hilal El Obied ya
Sudan,Raja Casablanca na Berkane za Morocco,Djoliba ya Mali,CR
Belouizdad ,USM Alger za Algeria,La Mancha ya Congo Brazaville na Supersport United ya Afrika Kusini.
Timu
ambazo zimetolewa Ligi ya Mabingwa na kuangukia Shirikisho ni Yanga ya Tanzania,Aduana
Stars ya Ghana,Al-Hilal Omdurman
ya Sudan,Rayon Sport ya Rwanda,ASEC Mimosas na WAC za Ivory Coast,Gor
Maria ya Kenya,As Vita Club ya DRC,Plateau United na
MFM FC za Nigeria,Generation
Foot ya Senegal,Bidvest Wits ya
Afrika Kusini,CF Mounana ya Gabon,St,George ya Ethiopia ,Zanaco
United ya Zambia na US Songo ya
Msumbiji.
Droo
ya ratiba ya mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho inatarajiwa kupangwa Leo majira ya saa 8:30 Mchana kwenye makao
makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Mjini Cairo huku inatarajiwa kuwa Live
kupitia ZBC2 kwa mjibu wa taarifa ya Shirikisho hilo
No comments:
Post a Comment