Uzinduzi
wa tawi la CRDB Chato uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Joseph Magufuli unadhihirisha Tanzania ya maendeleo ni lazima.
“Kujenga
standard gauge kwa shilingi trilioni 7.6 fedha za ndani, msifikiri watu
wanafurahi” “Tunapoamua kujenga Stigler’s Gorge ambayo itazalisha umeme zaidi
ya megawati 2100 usifikiri wanaweza kufurahi” ”Tunapoweza kununua ndege kwa
fedha zetu, kitu ambacho tulishindwa kwa miaka 50 usifikiri watu wanafurahi”
“Tunapoweza kulipa mishahara tarehe 21 usifikiri wengine wanafurahi”. Rais
Magufuli.
Maneno
hayo ya Rais yametokana na utekelezaji wa miradi mikubwa kadhaa ya maendeleo,
kupiga vita rushwa, uboreshaji wa huduma za jamii hususan elimu bure, afya,
usambazaji wa umeme, maji na matumizi sahihi ya fedha za Umma zimeipaisha Tanzania
kiuchumi.
Nina
hakika sio rahisi kumshawishi Mwingereza au nchi yeyote iliyobobea kwenye
uchumi mkubwa iwapo unafanya hovyo hovyo, eti akushabikie kuwa nchi yako uchumi
wake unamuelekeo mzuri na itafika mbali.
Lakini leo sio ajabu maana imetokea Tanzania ambayo
ina muelekeo mzuri wa uchumi na inatabiriwa kufika mbali kimaendeleo.
Penye
ukweli uongo hujitenga, Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika nchini
Uingereza Stewart Rory ameeleza namna alivyovutiwa na mabadiliko yanayofanywa
kwenye sekta ya elimu, kupitia sera ya elimu bure ambayo imewezesha kuwepo kwa
ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi.
Kufuatia
mabadiliko hayo Uingereza imetoa Paundi milioni 140 kusaidia maboresho katika
miundombinu ya utoaji wa elimu hususan ujenzi wa madarasa na nyenzo za
ufundishaji.
“Nimetembelea
shule za msingi na kushuhudia mabadiliko makubwa yaliyofanyika, ikiwemo utoaji
elimu bure. Tutatoa zaidi misaada kusaidia masuala ya kitaaluma, ikiwemo ujenzi
wa madarasa”. Amesema Rory.
Aidha,
Balozi wa ufaransa nchini Friederic Clavier alipokwenda kumtembelea Mhe. Samia
Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisini kwake
Jijini Dar-es-salaam, alisema kuwa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, anaunga
mkono juhudi za dhati zinazochukuliwa kuhakikisha uchumi wa Tanzania
unaimarika.
“Rais
wa Ufaransa anauhakika na Tanzania
ijayo na anaunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli”
amesema Clavier.
Naye,
Muwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwenye masuala ya Watoto
Profesa Virginia Gamba amesema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada za kudumisha
amani ndani na nje ya nchi.
Aidha,
amesema;“Tanzania ni
miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo
zinazopaswa kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa serikali
yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania”.
Pia,
Muwakilishi wa Benki ya Dunia katika nchi za Burundi,
Malawi
na Somalia Bibi Bella Bird tarehe 4 Desemba mwaka jana akiwa Ikulu Jijini
Dar-es-salaam, alimuhakikishia Rais Magufuli kuwa taasisi hiyo, imejipanga
kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
Hii yote ni kwa sababu ya usimamizi mzuri wa fedha za maendeleo ambazo
zinasimamiwa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli
Bibi Bird
amesema “2016 Benki ya dunia ilitoa mkopo nafuu yenye dhamani za Dola ya
Marekani bilioni 1.2, ambazo zilikuwa sawa na trilioni 2.7 fedha ya Tanzania. Fedha
hizi zimekwenda katika miradi mbalimbali na tunafurahi kuwa zimetumika vizuri kama ilivyokusudiwa’
Benki
ya Dunia imetoa kipaumbele katika miradi ya miundombinu ya barabara na reli,
kuongeza usambazaji na uzalishaji wa nishati ya umeme, tekinolojia ya habari na
mwasiliano, elimu, ili kuhakikisha idadi ya wanaopata elimu inaongezeka,
uboreshaji wa sekta ya afya, na kuongeza upatikanaji wa maji safi.
Akizungumzia
hali ya uchumi Wilayani Chato Rais Magufuli amesema;”Kwa sasa tupo kwenye
mstari sahihi nawaomba Watanzania mvumilie ili tufike mahali ambako Tanzania
itakuwa nchi ya asali”
Rais
Magufuli anamaanisha kuwa, Tanzania
itakuwa nchi ya asali kweli kutokana na mbio, kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano
hii ni dhahiri bila kificho. Mpaka sasa kila kitu cha maendeleo kinachofanywa
na Serikali kinawekwa hadharani ili kudhihirisha imedhamiria kutenda inachosema.
“Niliapa
kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani nataka tujenge uchumi wa kweli”
amesema Rais Magufuli.
Haiingii
akilini nje ya Tanzania
watu wanaona mbio za maendeleo zinavyoshika kasi hapa nchini, na kutabiri
matokeo yake kuwa ni ustawi wa nchi na watu wake. Lakini ndani ya Tanzania waone
ni mateso, kutoa maneno yasiyofaa na kutaka kufanya vitu vinavyovuruga amani,
upendo na mshikamano jambo hili tulikatae.
Vilevile,
Rais aliongeza kuwa Tanzania
ya viwanda imeanza kupatikana na kinachohitajika ni kuongeza juhudi bila kujali
vitisho na maneno ya kukatisha tamaa kutoka kwa yeyote ndani au nje ya nchi.
“Tunaposema
viwanda kuna mataifa yahapendi. Hata tukitaka kujenga viwanda vya nguo hawataki
kwa sababu wananufaika. Wanataka tulime Pamba kisha tuwauzie wao watengeneze
nguo kisha wazivae halafu watuletee mitumba”. Amesema Rais Magufuli
Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya madini, Royalty Exploration
Corporation (TRX) kutoka
Canada James Sinclair amesema;
“Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli amekaribisha wawekezaji zaidi
baada ya kupiga vita rushwa na udanganyifu katika mfumo”.
Aidha,
Sinclair aliongeza kwa kusema kuwa, Serikali imeweka mazingira mazuri ya
kiuchumi na kisiasa kuhusu uwekezaji nchini Tanzania. Ambapo kampuni yake imeingia
makubaliano na Wakala wa Madini Tanzania (STAMICO) miaka kadhaa iliyopita,
lakini haikuathiriwa na mabadiliko ya sheria, kwa kuwa walishaingia katika
mabadiliko ya ulipaji wa kodi.
Akizungumzia
suala la viwanda wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris
Tanzania Ltd, kilichopo mjini Morogoro, Rais amekuwa mwalimu mzuri na kutoa
somo kwa Watanzania kuwa kiongozi mzuri ni yule anayetatua kero na sio
anayetengeneza kero.
“Serikali
imejifunza kutokana na makosa ya hapo nyuma ya kuweka kodi kubwa kwenye
viwanda ambapo ilisababisha viwanda vingi kufa, sasa mazingira mazuri
yanawekwa ili kulinda viwanda hivyo”; amesema Rais Magufuli
Kitendo
ambacho kinashawishi wawekezaji wengi kuja Tanzania kuwekeza pamoja na wazawa
kama alivyofanya Philip Moris Tanzania Ltd na Mansoor, au kiwanda cha sukari
kinachotarajiwa kuzinduliwa ambacho kinajengwa na Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA).
Tumuunge
mkono Rais kwa kila jambo analotekeleza ili tuende sote kwa pamoja, tuweze
kutumia fursa mbalimbali za kazi, biashara na uwepo wa soko la uhakika la
Afrika Mashariki lenye idadi ya watu takribani milioni 200. Pia, soko lipo la
Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) 665.
Mafanikio
yote hayo yametokana na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma kwenye wa
miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ni gumzo ndani na nje ya Tanzania. Miradi
hiyo ni pamoja na mradi wa reli ya kisasa unaojengwa kwa fedha za ndani ni
mfano wa kuigwa Barani Afrika, Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda
hadi Tanga na mradi wa Umeme wa Stiglers Gorge wa Rufiji.
Miradi
mingine ni ununuzi wa ndege 6, ujenzi wa kiwanda cha kimiminika cha gesi Mkoa
wa Lindi, Mpango wa Elimu Bure, Mabasi ya mwendo kasi na Tanzania ya viwanda
kila Mkoa viwanda 100. Aidha ujenzi wa meli katika ziwa Nyasa, Victoria na
Tanganyika, Mpango wa umeme Kinyerezi 11, 111, usambazaji wa umeme vijijini,
upanuzi wa viwanja vya ndege na vita dhidi ya rushwa.
No comments:
Post a Comment