Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier
ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa
(AFD) Bw. Emmanuel Baudran.
Katika
mazungumzo hayo ambayo yamefanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi
Clavier amewasilisha salaam za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kusema “Rais
wa Ufaransa ana uhakika na Tanzania
ijayo na anaunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli”
Balozi
huyo mpya wa Ufaransa nchini ambaye amekutana na kuzungumza na Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala
mbali mbali ya Kimataifa na kusema “Tanzania ni nchi yenye utulivu na Amani
kitu ambacho kinaipa taswira nzuri Umoja wa Mataifa”.
Mhe.
Balozi amemjulisha Makamu wa Rais kwamba Ufaransa imekusudia kuimarisha
uhusiano zaidi na Tanzania
wa Uchumi na Siasa na kuanzisha majadiliano mbali mbali katika masuala ya
Mazingira,Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Balozi
Clavier amemjulisha Makamu wa Rais kuwa mwezi ujao kutakuwa na ugeni wa wafanya
biashara kati ya 30 au 40 kutoka nchi ya Ufaransa ambao watakuja kujionea fursa
mbali mbali za kibiashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Mhe.
Balozi amemuelezea Makamu wa Rais azma ya Ufaransa kushirikiana na Vyuo Vikuu
vya Tanzania
katika kuanzisha na kuendesha kozi mbali mbali kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mwisho
aliipongeza Serikali kwa mapambano dhidi ya rushwa na urasimu jambo litakalo
wavutia wawekezaji wengi nchini.
Aidha,
Bw. Emmanuel Baudran Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa
alisema Shirika lao linakusudia kuanzisha kiwanda cha vifaa vya umeme wa jua
(solar) mkoani Shinyanga pia shirika hilo
limeshafanya miradi ya uboreshaji maji taka katika manispaa ya Temeke na
wanaendelea na mikakati ya uanzishwaji wa miradi mingine.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan alimshukuru na kumpongeza Balozi wa Ufaransa kwa kazi nzuri wanazofanya
hapa nchini.
Alimhakikishia
kwamba Serikali ya Tanzania
ipo tayari kutoa ushirikiano kwa mambo yote muhimu yenye maslahi kwa wananchi.
Wakati
huohuo Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa
WFP nchini Mhe. Michael Danford.
No comments:
Post a Comment