Naibu Waziri Wa Nishati Subira Mgalu ambae pia ni
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani amekabidhi Mifuko ya Saruji Mia Tatu kwa
Viongozi wa Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga katika hafla fupi iliyofanyika
terehe 6/3/2018 Ikwiriri.
Msaada huo wa Saruji ni kwa ajili ya Ujenzi
unaoendelea kwa nguvu za Wananchi kwenye Vituo vya Afya Wadi za Wazazi Mloka na
Nyamwinywili kata za Mwaseni na Kipugira upande wa Wilaya ya Rufiji .
Aidha, kwa upande wa Wilaya ya Kibiti Saruji hiyo
inakwenda kutumika katika Ujenzi wa Kituo cha Afya Nyamatanga Rualuke na
Sekondari ya kata ya Dimani ambapo Mkuranga Mifuko hiyo itatumika katika ujenzi
wa Zahanati ya Kazole na Shule mpya ya Msingi Kisemvule.
Mhe Mgalu ametoa Msaada huo wa Mifuko 300 ya
Saruji kufuatia Ziara yake katika wilaya hizo Mwezi Desemba 2017 ambapo
alijionea ujenzi wa Miundombinu hiyo kwa nguvu za Wananchi na Wahisani
mbalimbali.
Kwa kutambua Umuhimu wa Wilaya hizo hasa maeneo
ambayo mradi Mkubwa wa Rufiji Hydropower utatekelezwa mfano Mloka Mwaseni ambapo
kuna haja ya kuwa na MiundoMbinu imara ya Huduma Wezeshi Mfano Zahanati na
Vituo vya Afya ili kuufanya Mradi utekelezeke Kirahisi na kwa Wakati .
Akizungumza na viongozi hao mara baada ya
kukabidhi msaada huo, Mhe Mgalu amewaasa Viongozi wa Maeneo hayo kusimamia vizuri
ili Saruji hiyo itumike kama ilivyokusudiwa .
Pia amewaomba Wadau Mbalimbali kujitokeza Kusaidia
Ukamilishaji wa MiundoMbinu hii kwa Maslahi ya wananchi wa Maeneo hayo.
Wakipokea Saruji hiyo waheshimiwa Wabunge wa
Maeneo hayo wamemshukuru Mhe Mgalu na Kumuahidi kuwa watahakikisha Saruji hiyo
itafanya Kazi iliyokusudiwa .
Viongozi hao akiwemo Mkuu wa Wilaya Rufiji Mhe
Juma Njwayo amempongeza Mhe Subira kwa kazi nzuri anazofanya na michango yake
ya Mara kwa mara katika Sekta mbalimbali .
Naibu Waziri Nishati alikuwa Wilayani Rufiji
kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Mradi mkubwa wa Rufiji Hydropower.
Naibu Waziri Wa Nishati Subira Mgalu, akimkabidhi Saruji Mhe. Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Mhe Abdallaah Ulega.
No comments:
Post a Comment