Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano
kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na
Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne
yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa
kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
..............................................
MAAFISA
Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini
wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za
utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala
yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.
Hayo
yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo
kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus
alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na
Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano
katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja
mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.
“Maafisa
Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi
wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari
ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu
ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.
Aidha,
alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza
taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya
wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma
mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Akifafanua
zaidi alisema Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika maeneo yao
ya kazi, hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao wa kazi kwa ajili
ya kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja mbalimbali zinazoulizwa na
kujitolea majibu kwa wakati.
Aliongeza
kuwa matumizi ya tovuti ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo wa
utoaji wa habari na taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa, hivyo ni
wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili kuhakikisha
kunakuwepo na daraja la mawasiliano baina ya Serikali na wananchi katika kupata
suluhu ya masuala mbalimbali ikiwemo migogoro inayotokea mara kwa mara.
Kwa
upande wake, Kiongozi wa Timu ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima
alisema uboreshaji wa tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dhana halisi ya
utawala bora hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na
Halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zinazozingatia
muda na mahitaji yaliyopo.
Aliongeza
ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu mwongozo
wa uandishi wa habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na Halmashauri
mbalimbali nchini kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa na Serikali yao
katika kuwapatia huduma mbalimbali.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya
uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro,
Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa
mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya
Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Afisa Tehama kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred Chali akichangia hoja wakati wa
mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya
Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne
Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji
Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada
la Marekani (USAID).
No comments:
Post a Comment