Naibu
waziri wa nishati Subira Mgalu, wa kwanza kulia na Mkuu wa wilaya ya bagamoyo
wa pili kushoto walipofika Chalinze kujionea aja;i ya moto ambayo imesababisha
vifo vya watu wanne.
....................................
Naibu
waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema serikali inasubiri uchunguzi wa tukio la
moto uliotokea Chalinze ambao umesababisha vifo vya watu wanne ili kuona ni
maelekezo gani ambayo inaweza kuyatoa.
Naibu
waziri huyo wa nishati aliyasema hayo jumatatu Mach 12, 2018 baada ya kutembelea katika eneo la tuki la
ajali ya moto katika halmashauri ya Chalinze.
Kauli
hiyo ya waziri imekuja kufuatia taarifa za awali ambazo zinaonyesha kuwa, moto
huo umesababishwa na hitilafu ya umeme saa saba za usiku wa jumamosi kuamkia
jumapili ya Mach 11, ambapo watu wanne wamefariki dunia na wengine wawili
kueruhiwa huku mtoto wa miaka miwili akiwa amenusurika.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga alimuagiza Afisa Tarafa ya
Chalinze kufanya tathmini ya namna ya kuwasaidia walionusurika katika ajali
hiyo katika kipindi hiki kigumu walinachonacho.
Naibu
waziri wa nishati Subira Mgalu, wa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
wa kwanza kushoto walipofika Chalinze kutoa pole kwa familia iliyopata ajali ya moto ambayo imesababisha
vifo vya watu wanne.
Muonekano
wa nyumba iliyoungua moto huko Chalinze
No comments:
Post a Comment