Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimkabidhi moja ya gari la wagonjwa aina ya
Suzuki Maruti, Ashura Nkya ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
ya Babati katika bandari ya Dar es
Salaam jana.
Baadhi ya magari aina ya Suzuki
Maruti ambayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamuru yagawiwe
katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhudumia Sekta ya Afya nchini.
.......................................
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),
Selemani Jafo, ameendesha zoezi la kugawa magari 50 ya wagonjwa aina ya Suzuki
Maruti (Ambulances) kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini Jijini Dar es
Salaam.
Magari
hayo ambayo awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli aliagiza yafanyiwe utaratibu wa kisheria wa kiforodha na
yagawanywe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili yatumike kwa kuwahudumia
wananchi katika vituo mbalimbali vya afya nchini.
“Hii
ni agenda ya Mhe. Rais ya kutaka kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora,
ambulance hizi ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana na zitatusaidia katika
halmashauri nyingi,”amesema Jafo.
Aidha,
Mhe. Jafo amemshukuru sana Rais wa John Magufuli kwa kuonyesha mapenzi makubwa
lakini pia amependezwa na Watumishi wa Wizara, Mikoa na Halmashauri zote
kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu iliyofanyika bandarini Jijini Dar es
Salaam.
Naye
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainabu
Chaula amemshukuru Waziri wa Nchi TAMISEMI na Waheshimiwa Wabunge wote kwa
utendaji wao na kuwataka wabunge kuwa na lugha ya ufahamu mmoja ili kuboresha
utendaji Serikalini.
“Kwa
niaba ya watendaji nawashukuru sana waheshimiwa Wabunge, nilitamani tutembee
pamoja kwa maana ya kuwa na uelewa wa pamoja na ndio maana Mhe.Waziri
amewakabidhi wabunge magari nao watukabidhi sisi,”Amesema.
Charles
Kichere Kamishna Mkuu wa Mapato Tanzania, amesema awali magari hayo aliyaona
Mhe. Rais alipofanya ziara bandarini na kwamba magari hayo yalikuwa
yameteleekezwa na mmiliki wake kutofahamika na ndipo rai, aliagiza kufuata
utaratibu wa forodha na kuyataifisha magari hayo na kasha yagawiwe kwenye
Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Kwa
upande wake Mhe. Prof Norman Sigalla King, Mbunge wa Makete, amemshukuru Mhe.
Rais kwa kutoa ambulance hizo kwa ajili ya kuimarisha huduma za mama
wajawazito.
“kwanza
nitoe shukrani za pekee kabisa kwa kupewa ambulance kwa ajili ya wilaya yangu
ya Makete nakumbuka niliomba kwa ajili ya tarafa za Ukutama, Matamba, Magomba,
Tulongwa na Niwaho”amsema.
Amebainisha
umbali wa kata ya Ukutama hadi Makete mjini ni kilomita 70 na hivyo itawanusuru
wakina mama dhidi ya vifo vya uzazi visivyotarajiwa.
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Hakimu Ndatama amemshukuru Mhe. Rais
kwa kuwapatia ambulance ambayo itaokoa vifo vya akina mama na watoto kwa kiasi
kikubwa.
No comments:
Post a Comment