Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza ameongoza mamia ya
waombolezaji kuaga mwili wa mwalimu John Mponda, ambae alikuwa Mkufunzi
Msaidizi daraja la 2, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Mwalimu
Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la
Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ( Bagamoyo International Festival of
Arts and Culture) .
Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Mwalimu John Mponda wa TaSUBa.
.................................................
Naibu
Waziri Habari, Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza amesema Wizara yake
itamkumbuka Mwalimu John Mponda kwani alikuwa kiunganishi kizuri kati ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na wizara yake katika
kufanikisha mambo mbalimbali ya Sanaa hapa nchini.
Naibu
Waziri huyo aliyasema hayo leo tarehe 21 Machi 2018 wakati wa kuaga mwili wa
mwalimu John Mponda shughuli zilizofanyika ukumbi wa TaSUBa Bagamoyo.
Alisema
licha ya kuwa Mwalimu marehemu Mponda Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,
(Bagamoyo International Festival of Arts and Culture) .
Alisema
wizara imempoteza mtu muhimu katika tasnia ya sanaa na kwamba mchango wake
utakumbukwa katika jamii.
Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) DKT.Herbert
Makoye amemualezea mwalimu Mponda kuwa ni mtu mchapakazi aliyekuwa akitoa
ushirikiano wa kila namna katika utekelezaji wa kazi za kiofisi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
alisema Mwalimu mponda ni mtu muhimu katika jamii hali iliyopelekea kila mmoja
aweze kushiriki mazishi yake.
Alisema watu wa Bagamoyo na wale wote waliopata taaluma ya
sanaa kupitia yeye watamkumbuka kwa jinsi alivyoweza kutoa ushirikiano wake
bila ya kubagua.
Nae Mtoto wa Marehemu Mary Mponda alisema kwa niaba ya familia
ya Mponda wanatoa shukrani kwa watu wote, TaSUBa na Serikali kwa ujumla kwa
namna walivyoweza kushiriki katika msiba huo wa baba yao.
Aidha, alisema kufuatia umati mkubwa ulifurika katika kumuaga
Mwalimu Mponda ni dalili tosha ya kuonyesha mapenzi makubwa waliyonayo kwa
marehemu huyo.
Mary alisema amepata fundisho kubwa kupitia msiba huo na kuona
ni jinsi gani mtu anapaswa kuishi na jamii ili kujenga mazingira mazuri
miongoni mwa watu na kwamba hilo atalichukua kama somo katika maisha yake.
Mwalimu
Mponda alizaliwa tarehe 10 Novemba 1963 wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe, aliajiriwa Chuo cha Sanaa
Bagamoyo (sasa TaSUBa) tangu Tarehe 10
Novemba 1984, hadi mauti yanamfika alikuwa na cheo cha Mkufunzi Msaidizi
daraja la 2,.
Aidha,
Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la
Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ( Bagamoyo International Festival of
Arts and Culture) .
Wakati
wa uhai wake Mwalimu Mponda aliwahi kuwa msanii katika kundi la "Bagamoyo
Players" lililokuwa linaundwa na wakufunzi wa TaSUBa, Bagamoyo Players
lilijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa kufanya maonyesho katika
nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kampeni mbalimbali za maendeleo.
Mwili wa Marehemu umesafirishwa kwendaMjini
Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya ambapo mazishi
yatafanyika tarehe 22 Machi 2018 hukohuko Wilaya ya Mbeya Vijijni.
Jeneza
liliobeba mwili wa Marehemu Mwalimu John John Mponda.
Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (wa pili kulia) wa kwanza kulia ni Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) DKT.Herbert
Makoye wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa, George Daniel Yambesi.
Baba
mzazi wa marehemu Mzee John Mponda watatu kushoto na wadogo zake marehemu
Mke
wa Marehemu Mponda wa pili kushoto na watatu kushoto ni mtoto wa marehemu, Mary Mponda.
Sehemu
ya umati wa watu waliofika Ukumbi wa TaSUBa kuaga mwili wa Mwalimu Mponda.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu,
Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo
Mshauri wa Mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja.....akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu,
Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
Mtendaji
Mkuu wa
Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)
Dr Siston Masanja Mgullah, akitoa heshima za mwisho
kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) DKT.Herbert
Makoye akitoa heshima za mwisho
kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
Meneja Mkuu wa Efm Radio Dennis Ssebo akitoa heshima za mwisho
kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
Watoto
wa Mwalimu John John Mponda wakiongozwa na dada yao
Mary Mponda wakati wakitoa salamau zao za mwisho kwa baba yao mpendwa katika Ukumbi wa TaSUBa.
No comments:
Post a Comment