Katika picha katikati kushoto
Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za
kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria
LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa
wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha
Mwakizega.
Chaga za kisasaa za kukaushia
dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani
Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria
LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe
nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu
katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah
Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza.
............................
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya
ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua
kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi
za mifugo.
Ulega
ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo
Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi
kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla,
kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka
niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia
jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji
katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa matatizo ya
wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana
kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika
uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji
basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema
Ulega.
Ulega
alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za
uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na
utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu
Waziri Ulega alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa
Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye
hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke
yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia
vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi
ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka”
Alisisitiza
Awali,
akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa
Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia
20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya
shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili
mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw.
Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa
elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ya
uvuvi.
No comments:
Post a Comment