LOWASA AHOJIWA NA KUACHIWA.

index
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.

Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU