Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya kuadhimisha siku
Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
Wanajopo
wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto
ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili
Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for
Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama
katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Mjadala
ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni
Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika
la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu,
wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada)
na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern
Energy Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika
kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia
mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto ni
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala mbalimbali
inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Kauli mbiu ya mwaka
huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
No comments:
Post a Comment