Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akipokea
Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter
Mshama Katika uwanja wa shule ya Sekondari
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj
Majid Mwanga ,amepokea mwenge Uhuru kutoka Kibaha, ambapo amesema utatembelea
miradi yenye thamani ya zaidi ya sh .bilioni 128.
Mwenge huo wa Uhuru umeanza kwa
katika Halmashauri ya Bagamoyo kwa kutem belea m iradi m balimbali ya maendeleo
Mwanga, alisema Bagamoyo ni ukanda
wa kiuchumi (Special economic zone) na hivyo kufanya Bagamoyo kuwa na viwanda
vingi.
Mradi mmoj umezinduliwa, minne imewekwa
jiwe la msingi na kutembelea vikundi mbali mbali vinavyojishughulisha na
shughuli za ujasiliamali.
Akipokea mwenge wa Uhuru shule ya
sekondari Lengo Trust ,mkuu huyo wa wilaya ,alisema wamejipanga kuinua uchumi
na kupiga maendeleo kupitia viwanda na fursa mbalimbali za kiuzalishaji.
Alhaj Mwanga alisema, wanapambana
na vitendo vya rushwa ,madawa ya kulevya pamoja na ugonjwa wa malaria na
maambukizi mapya ya ukimwi.
Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017, Amour Hamad Amour akizungumza katika shule ya Sekondari
Fukayosi alisema ni vyema wananchi wabagamoyo wakatunza miradi yote
iliyoanzishwa ili ilete manufaa kwa vizazi vya baadae.
Aidha, amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa ili
kufanikisha ujenzi wa shule nzuri kata ya Fukayosi ambayo i na maabara ya
kisasa na Darasa la Comptuter mpya.
Aliwaasa wanafunzi kufanya juhudi katika masomo
ili wapate elimu bora kama yaliv yo majengo yao.
Nae Diwani wa kata ya Fukayosi Ali Ali, aliwataka wananchi kutenga maeneo
kwaajili ya maendeleo ili hata akipatikana mfadhili iwepo sehemu ya kujenga.
Ali Ali ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bagamoyo alitoa wito kwa wananchi wa Halmashauri ya Bagamoyo kutumia fursa
zilizopo k atika miradi inayoendelea
Bagamoyo ili kujiletea maendeleo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitafa mwaka 2017, Amour
Hamad Amour akizungumza na wananchi katika shule ya Sekondari Fukayosi iliyopo
kata ya Fukayosi katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akimkabidhi
kiongozi wa mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour, Risalaya yake ili ifike kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge
katika Halmashauri ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment