Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Jimbo la Chalinze wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyomalizika jana mkoani Pwani
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akihutubia wakati wa ziara ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani jana.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyomalizika jana mkoani Pwani jana
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza juisi ya Sayona katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani jana.
...................
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli , amempongeza Mbunge wa
Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kwa kupiga hatua katika kusimamia
utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo lake.
Rais M agufuli ametoa Pongezi hizo alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani na kutembelea Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo
Ziara
hiyo ya Raisi ambayo ilikuwa na kazi ya Kufungua Miradi ilianza na ufunguzi wa
Kiwanda kikubwa cha matunda cha Sayona kilichopo Mboga Wilaya ya Chalinze.
Pamoja
na kumkaribisha Mheshimiwa Mbunge alimuhakikishia Mheshimiwa Raisi juu ya
KUMUUNGA mkono katika hatua anazochukua ikiwemo kupambana na Ufisadi na kuwahakikishoa
Watanzania kutawala Uchumi wao. Mheshimiwa Mbunge alimueleza juu ya jitihada
ambazo Wana chalinze wanazifanya kujikomboa katika Uchumi tegemezi.
Mheshimiwa
Mbunge alimueleza Mh. Raisi jinsi Halmashauri yao ilivyofanikiwa kukusanya
fedha kwa kuvuka kiwango cha makusanyo. " Mh. Raisi halmashauri yako hii
ya Chalinze imefanikiwa kukusanya zaidi ya Asilimia 102 juu ya makadirio mbayo
tulikuwa tumejipangia.
Fedha hizi zitapelekwa katika miradi ambayo inagusa
wananchi wa chini kabisa ikiwemo kuimarisha huduma za afya, maendeleo ya jamii,
mikopo kwa wakina mama na vijana na pia miradi ya maji kwa ajili ya kupunguza
makali.
"Mh.
Raisi , tumejipanga pia kuhakikisha kuwa halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe.
Zaidi ya Milioni 200 zimepelekwa kuwasaidia wananchi maskini kimikopo na
shughuli za maendeleo kwa ushirikiana na wadau wa maendeleo tumefanikiwa
katika haya." Mbunge alieleza.
Pia
mbunge alimuomba Mh. Raisi kutumia Chalinze kama sehemu ya ushuhuda wa hatua na
jitihada anazochukua kukuza uchumi wa watu na maendeleo ya kweli yanayotazama
uelekeo wa kiilani na ahadi zake.
Mheshimiwa Mbunge alimueleza Mheshimiwa Raisi
kuwa ," kama yupo mtu ambaye ana shaka na utayari wako na uchapakazi wako
juu ya sera ya viwanda basi Mwambie aje Chalinze aje kuona jinsi mambo yanavyofanyika."
Tunajua wewe ni kazi tu na sisi hapa chalinze ni kazi tu. "
Mheshimiwa
Raisi alimshukuru Mbunge na kwa hakika alimpongeza kwa kumfananisha na Baba
yake Aliyewahi kuwa Raisi Wa Jamhuri ya Tanzania wakati wa awamu ya Nne.
Mheshimiwa Raisi alimfananisha na Nyoka mtoto. "Kwa hakika nimemsikia
Mbunge wenu na nimeridhika kuwa Nyoka uzaa Nyoka".Nimekuona na
ninakupongez unavyochapa kazi. Hongera sana ."
Pamoja
na kumshukuru mbunge , Mheshimiwa Raisi aliwakabidhi Halmashauri ya Chalinze
majengo ambayo yalitumiwa na Mkandarasi pale Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara
ya Bagamoyo-Makofia-Masata.
Baada
ya kumaliza mkutano huo na kufungua kiwanda cha kuchakata Matunda cha Sayona,
Mheshimiwa Raisi alielekea katika Halmashauri ya Bagamoyo ambako alifanya mambo
mawili makubwa ikiwemo uzinduZi wa Barabara ya Bagamoyo Msata na Kiwanda cha
kukausha Matunda kilichopo Mapinga, Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment