Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,mkoani Pwani imepiga marufuku uingiaji na
uchinjaji wa nguruwe ili kukabiliana na ugonjwa wa homa ya nguruwe African
Swine Fever,ambao unadaiwa kuingia .
Tangu ugonjwa huu uingie jumla ya nguruwe 71 wameshakufa na baada ya
kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale
waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo.
Ofisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa wa Kibaha ,Innocent Byarugaba
alipozungumza na mwandishi hizi alisema halmashauri hiyo pia imezuia kuingiza
nguruwe .
Byarugaba alieleza ugonjwa huo uliingia mwanzoni mwa mwezi may kwenye
kata mbili za Picha ya Ndege na Viziwaziwa eneo la Mikongeni.
“Wananchi wawe na tahadhali ,ugonjwa huu tayari umesababisha vifo vya
nguruwe 71 na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama
hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo,” alisema
Byarugaba.
Alisema hatua za awali zilizochukuliwa ni pamoja na kuzuia nguruwe kuingia na
kutoka katika maeneo yaliyokuwa na viasharia .
“Sampuli mbalimbali za nguruwe waliokufa zilichukuliwa na kupelekwa
maabara kuu ya mifugo Temeke Jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi na kubaini
uwepo wa ugonjwa huo ,” alisema Byarugaba.
Hata hivyo ugonjwa wa African Swine Fever,ambao unadaiwa
kuingia kwa nguruwe hauwezi kuambukiza binadamu ila madhara yake makubwa
ni kuteketeza nguruwe wengi asilimia 100,kwa muda mfupi na kusababisha hasara
kwa mfugaji.
Byarugaba alitaja dalili za ugonjwa huo ni kuvuja na kusambaa kwa damu
kwenye viungo vya mwili , homa kali, kupumua kwa shida, kutapika, vifo ndani ya
siku mbili hadi 10 na muonekano wa damu kuvilia kwenye viungo mbalimbali vya
ndani vya nguruwe baada ya kumpasua.
Alieleza kufuatia ugonjwa huo ,idara ya mifugo na uvuvi katika
halmashauri ya mji wa Kibaha ,wataalamu wake inatoa elimu kwa wafugaji ili
kudhibiti,kwa kupita kata na mitaa .
Ugonjwa huo hushambulia nguruwe na hauna tiba kwa wanyama wanaoupata na
husababisha vifo vingi unapotokea hasa kwa wanyama wakubwa.
No comments:
Post a Comment