Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha mjadala
wa Bajeti ya Wizara yake ambapo Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Naibu wake
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za Wabunge
wakati wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Bunge hilo
limepitisha Bajeti ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya
wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada
ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752
kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mkurudenzi
wa Idara ya Mipango-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (kulia),
akipongezana na Mkurugenzi wa Bima ya Taifa, kwenye viwanja vya Bunge Mjini
Dodoma baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akimsikiliza
kwa makini Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni nje ya Ukumi wa Bunge mara
baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752
kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Gavana
wa Benki Kuu (BOT), Prof. Beno Ndullu (kushoto), akimpongeza Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha makadirio
ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa
Fedha 2017/2018 Mjini Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipeana mkono na Mkaguzi
Mkuu wa ndani wa Serikali Bw. Mohamed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini
Dodoma baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni
11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoro) akimshukuru
na kumpongeza Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi kubwa
aliyoifanya katika kusimamia na kuhakikisha kuwa Bajeti ya Wizara hiyo
inaandaliwa kwa viwango vya juu na hatimaye kupitishwa na Bunge Mjini Dodoma
ambapo Wizara hiyo imeidhinishiwa kukusanya nakutumia shilingi trilioni 11.752
kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa saba
kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu
wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Mjini
Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti wa Wizara hiyo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment