Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipokea beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem.
Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo
watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem.
Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo
watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi. (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
......................
Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi
zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara
na Zanzibar.
Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam
ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi
hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza
mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.
Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya
kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi
milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali
nchini.
Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya
Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa
Tanzania Bara na Zanzibar.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema msaada huo utasaidia sana
wanawake wajawazito na waliojifungua kupata vifaa za uzazi ambavyo vinahitajika
wakati wanamke mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa vifaa hivyo
vitaanza kusambazwa kuanzia mwezi huu na mchakato wa kuainishwa hospitali
zitakazopata msaada huo unaendelea.
Makamu wa Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo
kati ya nchi ya Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande
zote Mbili.
Aidha Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemhakikishia
Makamu wa Rais kuwa Serakali ya Kuwait itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania
katika uimarishaji wa sekta ya afya na elimu nchini ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma bora na za msingi.
No comments:
Post a Comment