Mbunge
wa Chalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete (Kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza wakati wa hafla ya
kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji
safi kutoka mto Wami pamoja na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la
Chalinze. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza kwa niaba ya Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya
kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka
ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze, Mhandisi Christer Mdomba, kulia ni Mkuu
wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa
DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangingo (Kulia) akitoa
maelezo ya utekelezaji wa mradi kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja
na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze.
......................
Takriban wakazi 234,398 wa
Chalinze watanufaika na mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa
mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi
unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi
huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa
Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumtaka mkandarasi
kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.
“Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana tumeweka wataalamu wetu
hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi kwa ubora na kwa kasi kama
ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi huu mwezi Machi mwaka huu”,
alisisitiza Lwenge.
Akifafanua, Mhandisi Lwenge amesema
kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya tatu ni
ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi wa matanki 19,
na ujenzi wa mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea.
Kazi nyingine zinazoendelea katika
kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji ambapo vituo 27
vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na vituo 98 havijaanza
kujengwa.
Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na
mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa ni kuongezeka kwa
upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi, kuongeza wafanyakazi na
maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni anayeweza kutoa maamuzi kwa
niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.
Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa
Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo kulipia malipo
ya huduma (service charge) hata pale wanapokuwa hawajapata huduma hiyo
ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi kulipia huduma pale
wanapotumia tu na si vinginevyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo
hilo, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema yeye binafsi anaishukuru Serikali ya Awamu
ya Tano kwa namna inavyoshughulikia changamoto zinazowakabili wananchi wa
Jimbo hilo ikiwemo ya maji.
“Naridhika na hatua iliyofikiwa katika
utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi huo ambao ukikamilika utasidia kwa
kiwango kikubwa kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo hili
hivyo wananchi wataweza kuongeza kasi katika shughuli za maendeleo”,
alisisitiza Ridhiwani.
Akifafanua amesema anaunga mkono juhudi za
Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo .
Mnamo
mwezi Machi mwaka huu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea mradi huo na kukagua shughuli
za ujenzi wa miundombinu ya mradi huo Awamu ya Tatu na baada ya
ziara aliagiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo ambaye ni Overseas Infrastracture
Alliance (OIA)Pv
Ltd kutoka India mwenye ubia na Kampuni ya Pratibha
Industries nayo ya India kukamilisha kazi hiyo ,mkandarasi wa mradi huo
ameshalipwa shilingi 38,716,375,627 ikiwa ni asilimia 42 ya gharama ya mradi.
Uhaba
wa maji safi na salama umelikumba jimbo la Chalinze kwa kipindi kirefu. Kwa
sasa wanaopata huduma ya maji safi na salama ni 220,241, mradi ukikamilika, watakaopata
huduma hiyo watafikia jumla ya 234,394.
Moja
ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni
sehemu ya mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la ChalinzeChalinze, Mhe.
Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment