mmoja wa wakulima wa eneo hilo Asmaa Mshindo Msigala, ambae.
alimuomba Rais awasaidie kupata eneo ambalo wamekuwa wakilima kwa miaka mingi.
..........................
Rais la wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli ameridhia ombi la wananchi na wakulima wa sanzale/Kigongoni kuendelea
kuwepo kulitumia eneo hilo kwa shughuli za kilimo na makazi kama walivyozoea
kwa miaka mingi.
Akizungumza mbele ya Mh. Rais, mkulima eneo la
Sanzale Wilayani Bagamoyo, mmoja wa wakulima wa eneo hilo Asmaa Mshindo Msigala alisema kwa muda mrefu wamekuwa
wakitumia eneo hilo kama sehemu yao ya kulima na kwamba mwaka huu wameshindwa
kuendelea na kilimo na shughuli mbalimbali kutokana na askari magereza kuwazuia
wananchi hao kufanya shughuli zozote ndani ya
eneo hilo.
Bi Asma Msigala kwa niaba ya wakulima wa Sanzale
amemuomba muheshimiwa Rais kuwafikiria ili ikiwezekana kuwaachia eneo hilo ili
waendelee na shughuli zao kama kawaida.
Kufuatia hali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameridhia
ombi hilo na kumuagiza mkuu wa Gereza la Kigongoni Muyengi Bulilo kuwaachia
wananchi hao eneo lenye ukubwa wa heka 65 kwa
shughu li za kiraia.
Awali Rais, Dkt.
Magufuli alimuuliza mkuu wa Gereza
la Kigongoni, Muyengi Bulilo kama eneo
lote la Gereza la Kigongoni lina ukubwa
gani ambapo mkuu wa Gereza alisema eneo la Gereza l a Kigongoni lina ukubwa
zaidi ya heka 6000.
Rais Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa kuanzia leo Juni 22, 2017
amewakabidhi rasmi eneo hilo na kwamba
mpaka wa Gereza na wananchi utakuwa ni Barabara ya Msata ambapo Ukitoka Bagamoyo Kushoto ni eneo la Magereza na Kulia ni
eneo la wananchi.
Kwa muda mrefu wananchi na wakulima wa eneo la
Sanzale wamekuwa wakilalamika kwa kupata usumbufu kutoka kwa askari magereza
pindi wanapotaka kufanya shughuli zao
katika eneo hilo.
Aidha, Rais Magufuli pia alimpongeza mkuu wa Gereza la Kigongoni kwa kuridhia eneo hilo kuwaachia
wananchi.
Rais Dkt. John Magufuli alikuwa akizungumza na wananchi
katika eneo la Sanzale Bagamoyo wakati wa
ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata yenye urefu wa kil omita 64
kiwango cha Lami.
Rais
la wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
Baadhi ya wananchi na wakulima wa eneo la Sanzale wakiwa katika moja ya mikutano yao kujadili namna ya kupata eneo hilo.
Baadhi ya wananchi na wakulima wa eneo la Sanzale wakiwa katika moja ya mikutano yao kujadili namna ya kupata eneo hilo.
Baadhi ya wananchi na wakulima wa eneo la Sanzale wakiwa katika moja ya mikutano yao kujadili namna ya kupata eneo hilo.
Hili ni moja ya majengo ambayo yaliwekwa alama ya kutakiwa kubomolewa ili iku pisha eneo lamagereza kama inavyoonekana.
No comments:
Post a Comment