Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo Alhaji, Majid Mwanga aliyevaa Kanzu, akizindua kisima kitongoji
cha Mto wa Nyanza, kata ya Kiromo, katikati ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Mto wa
Nyanza, Omari Said Salum na wa kwanza kulia
ni Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga.
Mkuu wa wilaya
ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga ameishukuru Taasisi ya Dhi Nureyn
Islamic Foundation yenye makao yake makuu mjini Iringa kwa kuchimba visima katika wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa
visima vitatu kata ya Kiromo, Mkuu huyo wa wilaya amesema Taasisi za dini
zinamchango mkubwa katika kuleta
maendeleo katika jamii.
Alisema
licha ya kufanya kazi za kiroho lakini pia zimekuwa mstari wa mbele
kusaidia huduma za kijamii kama vile ujenzi wa
visima, ujenzi wa Hospitali na shule, na kuongeza kuwa, hilo ndio lengo
la serikali kusajili taasisi
za dini pamoja na kutoa huduma za kiroho lakini pia zisaidie
kuleta maendeleo.
Aliongeza kuwa uwepo wa Taasisi za dini ni muhimu
katika jamii, kwani husaidia kuwajenga wananchi katika misingi ya imani, kumtambua Mungu na kuwajengea hofu juu ya kutenda maovu mbalimbali ikiwemo
uhalifu na badala yake jamii inahimizwa
kudumisha amani kutokana na imani zilizopo miongoni mwa wana dini.
Akii zungumzia Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foun dation, Mkuu huyo wa wilaya ya B aga mo yo ,
alisema Taasisi hiyo kwa muda mfupi toka i an ze kusaidia B agamoyo
imeweza kufanya mamb o makubwa kiasi ambacho inastahili kupongezwa.
Alisema Taasisi hiyo kwa sasa imeshac himba visima
10 wilayani Bagamoyo vyenye
thamani zaidi ya shilingi milioni mia moja
na kujenga wodi ya kina ma ma katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo ye
nye uwezo wa kukaa vitanda 40 pamoja na
jengo la mapokezi ya wagonjwa mahututi.
Mratibu wa miradi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Iddi Musa aliwataka wananchi wa waliopata
visima katika maeneo yao kuvitunza visima hivyo ili waendelee kufaidika na huduma hiyo ya maji huku thawabu
zikiwafikia wale waliotoa.
Nao wananchi wa kata ya Kiromo wamemshuku mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo kwa kuwatafutia
wafadhili wa kuwachimbia visima ili waondokane na adha ya
kutafuta maji umbali mrefu.
Walisema awali walikuwa wanapata tabu kutafuta maji na kulazimika kuchota maji kwenye mabwawa hali iliyokuwa
ikihatarisha afya zao pamoja na usalama wao.
Diwani wa kata ya Kiromo Hassan Usinga, akijaribu kufungua maji wakati wa uzinduzi huo wa visima katika kata yake.
Mratibu wa miradi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Iddi Musaakizungumza katika uzinduzi huo.
wananchi wa kata ya Kiromo waliojitokeza katika uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment