Rais wa J amhuri ya Muun gano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekemea tabia ya urasimu inayofanywa na
baadhi ya viongozi dhidi ya wawekezaji.
RAIS Dkt. Magufuli, ameyasema hayo wakati wa kuzindua kiwanda cha
vifungashio (global packaging co. ltd) kilichogharimu bil.8 ,na kiwanda cha
kutengeneza nondo cha Kiluwa chenye thamani ya bil.200, vilivyopoKibaha,Pwani.
Aidha amekemea baadhi ya taasisi zinazoweka mazingira ya rushwa na
urasimu wakati wa kutoa vibali kwa wawekezaji ikiwemo OSHA,NEMC na shirika la
viwango TBS.
Dk.Magufuli ,pia amezitaka taasisi za kifedha kukopesha watanzania
wazalendo na wale wenye nia ya kuwekeza kwa manufaa mapana ya taifa.
Hayo aliyasema wakati akizindua viwanda vya global packaging ,cha nondo
-Kiluwa na kuzindua na kufungua kiwanda cha kuunganisha matrekta ya Ursus.
Dk.Magufuli ,alisema ukosefu wa dhamana kwa wawekezaji linadidimiza kasi
ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya ukuaji wa uwekezaji na ujenzi wa
viwanda .
Rais Magufuli ,alieleza kwamba ,suala la vibali ameliona na anataka
asikie kuna mwekezaji amebaniwa kibali ,ili amshughulikie .
“Hili nilishaliona ndio maana vibali vya NEMC ,vimefutwa na kupitishwa na
bunge katika bajeti 2017/2018 ” alisema dk.Magufuli .
Dk.Magufuli alielezea kuwa ,kuna mabank zaidi ya 53 yalikuwa hayakopeshi
wawekezaji ,yalizoea kufanya biashara na serikali huku wenye madaraka na
wakubwa walikuwa wakitumia vibaya upenyo huo .
“Serikali ilikuwa inajila yenyewe ,nilipozibana ,kama Tanesco nilizuia
,bima ya afya na nyingine ,wakashtuka nikajua aaah nimegusa penyewe “
Aliipongeza bank ya TIB kwa kuamua kuikopesha kiwanda cha vifungashio
,alimpongeza mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,kwa kasi anayoenda
nayo na waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage.
Dk.Magufuli alisema ,kutokana na upungufu wa vifungashio kiwanda hicho
,kitasaidia wavuvi ,wazalishaji wa madini ,viwanda na wakulima kununua kwa gharama
nafuu ndani ya nchi .
Alisema soko la vifungashio lipo ,ndani ya SADC ,Tanzania na nje ya nchi
na ataendelea kukiunga mkono kiwanda hicho .
Akizindua kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus ,rais huyo ,aliitaka
NDC iwe mpya yenye kutoa matunda kitaifa ,sasa inafanya kazi na kuondoa ndoto
yake ya kuifuta kwani inaenda kwa kasi yenye matumaini .
Dk.Magufuli alisema mradi wakuunganisha matrekta ameubeba kwani
yatasaidia wakulima.
” Kilimo ni shughuli inayofanyika kwa asilimia 80,wananchi wanategemea
kilimo ,wengi wanatumia kilimo cha jembe la mkono hivyo matrekta itasaidia
kupunguza tatizo hilo.”alisema.
Kwa mujibu wake ,waangalie bei tofauti na matrekta yanayoagizwa nje ya
nchi ili yaweze kununuliwa na watanzania .
Alisema wakopeshwe wakulima kwa gharama nafuu .
Alieleza kwamba ,serikali imeanza kutoa utitiri wa kodi kwa asilimia 80
za kilimo ,asilimia 7 kwenye ufugaji na tano kwenye uvuvi ili viwe na mvuto na
kuendelea na biashara .
Alisema eneo la pembejeo limeoza na wameanza kulifuatilia,kuna pembejeo
hewa ,madudu ndani ya pembejeo wengine walishakufa wala hawana mashamba lakini
wameandikiwa wamepata pembejeo hizo.
“Tutatoa hatua ,hatujanyamaza ,hewa ni nyingi ,wapo walioandikishwa
watu hewa 56,000 Tasaf na pembejeo wapo ” sitolivumilia”
Hakusita kusema Tanzania ina urafiki mkubwa na nchi ya Poland na
amewahakikishia Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji .
Akizindua kiwanda cha chuma cha -Kiluwa ,aliwaomba wataalamu wa wizara
kuangalia kwa faida pana uwezekano wa kutumia chuma iliyopo nchini kuliko
kununua nje .
Alimpongeza Mohammed Kiluwa kwa kuzalisha nondo yenye kiwango na kuungana
na wawekezaji wa kichina.
Lakini aliitaka wizara husika na wawekezaji kununua chuma Liganga na
Mchuchuma maeneo yaliyopo nchini kuliko kununua China .
Katika hatua nyingine ,aliwaasa wawekezaji ,kujali maslahi ya wafanyakazi
na mikataba yao .
Dk.Magufuli, alisema wafanyakazi ndio wanaoongeza mali ya wenye mali
hivyo ni lazima kuwapa motisha ili wafanyekazi kwa bidii .
Nae waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Mwijage ,alisema nchi nzima
ina viwanda vya vifungashio 20 mojawapo ikiwa global packaging .
Alisema mkoa wa Pwani ,unaongoza kwa viwanda mbalimbali nchini ,ikiwemo
vitano anavyovizindua ,kufungua katika ziara yake .
Mwijage alieleza kuwa ,kujenga na kulinda viwanda ni majukumu yaliyochini
yake na anaahidi kuvilea .
Alisema ,viwanda hivyo vitawezesha ajira hasa kwa vijana na kuongeza pato
la Taifa .
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa ,alisema barabara ya
Mzenga -Makofia ni kero kubwa hivyo aliomba kuangaliwa kwa jicho la karibu iwe
kwa kiwango cha lami .
Alisema barabara hiyo itarahisisha usafiri kwa kiasi kikubwa .
Jumaa alieleza kuwa ,wawekezaji wakifika eneo lolote wanaangalia
miondombinu ya barabara .
Mbunge huyo ,alisema anasumbuliwa na wananchi ,km .5 ambayo ni ahadi yake
aliyoitoa wakati wa kampeni .
Alimuomba rais kuangalia kwa namna ya pekee Kituo cha afya cha Mlandizi
,kipandishwe hadhi kuwa hospital ya wilaya .
Jumaa alisema ameshaanza kujenga uzio wa utakaogharimu Mil.200 ambao
utasaidia kusukuma kigezo cha kupandishwa hadhi kituo hicho .
Awali ,mwanzilishi wa kiwanda cha global packaging, Joseph Wasonga
,anasema kiwanda kipo ubia na NDC ambapo kiwanda kina asilimia 94 .
Alisema kiwanda hicho kwa mwaka kitazalisha vifungashio milioni.16 .
Wasonga alitaja changamoto ya ukosefu wa dhamana kwa
wawekezaji unapofikia hatua ya kwenda taasisi za kifedha ,riba kubwa na tatizo
la vibali .
Wasonga ,aliishauri serikali na bank kuu kusimamia suala hilo ili
kuwapunguzia makali wawekezaji.
Alisema kwasasa wameshaajiri wafanyakazi 110 kati yake 109 ni wazawa
,malengo yao ,ni kuzalisha mara mbili ya sasa .
Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa,Mohammed Kiluwa alimwambia Rais,mkoa
huo,umejipanga kujiinua kiuchumi .
Aliomba kwa rais ,kupewa ardhi nyingine ili aweze kujenga viwanda vitano
kwa kushirikiana na marafiki zake wa kichina.
Kiluwa alisema,mradi huo mkubwa utazalisha zaidi ya tani 2,000 na kuajili
watu 300-800.
No comments:
Post a Comment