Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga
amewaonya wale wote watakaofanya fujo siku ya siku kuu katika mji wa Bagamoyo.
Akizungumza nyumbani kwake mara baada ya
kufuturisha, Alhaj Majid alisema skiku kuu ya Eidi ni siku kuu ya kidini na
kwamba tayari uislamu u meshatoa maelekezo juu ya kusherehekea siku kuu hiyo.
Alisema kumekuwa na tabia siku za siku kuu katika mji wa Bagamoyo kuja vijana kutoka nje
ya Bagamoyo kufanya fujo na hivyo kusababisha uharibifu wa mali
na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa
vitendo hivyo havitavumiliwa.
Mkuu huyo wa wilaya ambae pia ni Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, alisema ulinzi umeimarishwa
katika maeneo yote ya wilaya ya Bagamoyo hasa katika fukwe za Bahari ambapo makundi ya wageni yamekuwa
yakifika huko na kufanya fujo.
Alichukua nafasi hiyo kumuagiza mkuu wa Polisi
wilaya ya Bagamoyo, kuhakikisha wale wote watakaohusika na vurugu siku ya Eidi
wana chukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo viovu vya uvunjifu wa amani katika siku za siku
kuu.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku Disco
toto ndani ya wilaya ya Bagamoyo katika kipindi
chote cha siku kuu nakuwataka wazazi kuwa na karibu na watoto wao ili
kuwaepusha na madhara yanayotokana na burudani
ambazo zipo juu ya umri wao.
Aliwataka wazazi kuhakikisha watoto wanatembea
maeneo salama na kurudi nyumbani mapema.
MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ANAWATAKIA WANANCHI WOTE NDANI YA WILAYA YAKE SIKU KUU NJEMA YA EID EL FITRI.
No comments:
Post a Comment