Posts

RMO KAGERA ATENGULIWA KWA KUZUILIWA MWILI WA MTOTO MCHANGA KWA MADAI YA DENI LA MATIBABU HOSPITALINI.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba. Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amemwagiza katibu mkuu wa TAMISEMI nchini kutengua nafasi ya mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Issesanda Kaniki baada ya hospitali ya rufaa ya Bukoba ya mkoa huo kuzuia mwili wa mtoto mchanga kwa muda wa siku mbili kutoruhusiwa kwenda kuzikwa wakati wakijua watoto wanatibiwa bure. Maagizo mengine ameyatoa kwa viongozi wa serikali, siasa na watumishi mbalimbali nchini. Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo  Desemba 15, mwaka huu wa 2023, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kinachokarabatiwa ambapo pia alishuhudia utiaji wa saini ya mikataba ya usanifu miradi ya uboreshaji wa miundomninu ya miji Tanzania (TACTIC) kwa miji 15 ya kundi la pili. Ameagiza katibu mkuu TAMISEMI kwa kushirikiana na sekta ya afya kufanyika mapitio ya menejimenti nzima ya hospitali hiyo na kutoa maamuzi kwani alipata malalamiko ku...

POLISI KAGERA WAKAMATA SILAHA 11. NA RISASI 115.

Image
  Na Alodia Babara Bukoba. Jeshi la polisi mkoani Kagera limekamata silaha 11 zikiwemo bunduki 2 aina ya AK 47 zikiwa na magazine tatu, risasi 115, bastola aina ya glock 17 na bunduki aina ya gobore. Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP. Blasius Chatanda, akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 14, 2023, amesema kuwa, jeshi hilo  linaendelea kufanya oparasheni mbalimbali na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi katika mkoa huo ambapo katika oparasheni iliyofanyika kuanzia Septemba, 2023 hadi sasa silaha 11 zilikamatwa. “Katika kudhibiti matukio ya utekaji  nyara hasa kwa wafugaji katika mkoa wetu wa Kagera tumefanikiwa kukamata watuhumiwa 14 wa utekaji, tumekamata silaha mbili aina ya AK 47 zikiwa na magazine tatu pamoja na risasi 115 na bastola aina ya grock 17” amesema Chatanda. Aidha amesema katika kudhibiti matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha na ujagili jumla ya bunduki nane aina ya gobore zimekamatwa na kati ya hizo nn...

WAHITIMU ADEM WAPEWA SOMO NA PROF. MKENDA.

Image
  Wahitimu katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa elimu ­(ADEM) wametakiwa kwenda kusimamia vyema taaluma ya uongozi na utawala katika maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali katika maboresho ya elimu hapa nchini. Katika Mahafali ya 31 ya waahitimu hao yaliyofanyika tarehe 01 Desemba 2023, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema katika kipindi hiki cha mageuzi ya elimu, serikali inawategemea sana walimu hasa waliosomea uongozi na utawala katika kuhakikisha yale yote yanayotakiwa kuboreshwa yanasimamiwa  ipasavyo. Amesema tayari serikali inaendelea na mchakato wa maboresho ya elimu nchini kwa kuangazia mambo saba muhimu ambayo ni sera ya elimu, mabadiliko ya sheria ya elimu ya mwaka 1978 ambapo sasa elimu ya lazima ni miaka 10 kwa kila Mtanzania. Prof. Mkenda ameongeza kwa kusema kuwa, katika maboresho hayo , kuna marekebisho ya mitaala, kuwa na walimu, wakufunzi na wahadhiri kwa mgawanyo uliokuwa sawa,...

MAAMBUKIZI YA MALARIA KAGERA YAFIKIA ASILIMIA 18.

Image
  Na Alodia Babara  Bukoba.  Misimu miwili ya mvua ya vuli na masika inayonyesha mkoani Kagera imetajwa kama sababu ya mbu kuzaliana na hivyo kusababisha kiwango cha maambukizi ya malaria kufikia asilimia 18,  mkoani humo huku kiwango cha taifa kikitajwa kuwa ni asilimia 8. Kufuatia kiwango hicho kuwa juu, wilaya mbili za Karagwe na Kyerwa ambazo ziko pembezoni na vijiji viko umbali wa kuanzia kilomita tano kufika katika vituo vya afya wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 38 wamepewa vifaa tiba. Akizungumza leo Novemba 30,2023 katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kutolea huduma za tiba katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo mkurugenzi wa mradi wa Shinda malaria Dk Dunstan Bishanga amesema wahudumu hao walipewa mafunzo ya awali jinsi ya kupima joto na kuwaelimisha wanachi juu ya matumizi sahihi ya vyandarua. “Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa mitatu hapa nchini yenye maambukizi ya juu ya malaria ambapo watu 18 kati ya watu 100 wameathirika na vimelia vy...

EDU KWANZA WATOA FURSA YA MASOMO KWA VYUO VIKUU VYA CANADA & USA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA

Image
  Na Andrew Chale, Dar es Salaam. EDUKWANZA Consultants Limited ambao ni Mawakala wa Vyuo vya nje ya Nchi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ushauri huduma za Wanafunzi ya ILLUME imeendesha zoezi kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata fursa za masomo katika Vyuo vya nchi za Canada na Marekani (USA) tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam mapema leo Novemba 15,2023. Akizungumza katika tukio hilo lililowakutanisha wanafunzi mbalimbali waliofika kupata muongozo sahihi wa Vyuo vya nje, Mkurugenzi wa Edukwanza, Bw. Sarfraz Kassam amesema taasisi yao hiyo ina ushirikiano na Vyuo zaidi ya 500 Duniani ikiwemo Vyuo hivyo vya Canada na Marekani. "Edukwanza Consultants Limited leo Novemba 15,2023 tumefanya maonesho ya kuvinadi Vyuo vya Canada na Marekani katika mpango wa ‘Study in Canada & USA Fair 2023 ambao unasaidia kutoa fursa kwa in wanafunzi kusoma nje. Wanafunzi mbalimbali wa Tanzania wamefika na kupata ushauri kutoka kwa Wawakilishi wa vyuo hivyo vya nje, wakipata ushauri wa ...

UNESCO, WADAU WAKUTANA DAR KUJADILI UKATILI NA UNYANYASAJI KWA WENYEULEMAVU VYUO VYA UFUNDI NCHINI

Image
  Na Andrew Chale, Dar es Salaam. SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekutana na Wadau Wataalam kutoka mashirika yasiyo ya Kiserikali, Serikali na Mashirika ya watu wenye Ulemavu kupitia na kutolea maoni nyenzo za kukabiliana na vitendo vya kikatili na kinyanyasaji kwa wanafunzi walemavu wanaosoma Vyuo vya ufundi hapa nchini. Mkutano huo wa siku mbili yaani Novemba 14- 15,2023 mbali ya Tanzania, pia unafanyika sambamba katika nchi zingine tatu za Namibia, Msumbiji na Zimbabwe kwa pamoja wakijadiliana kupitia video kwa mtandao wa ZOOM.   Mkutano huo ni mpango unaotekelezwa na UNESCO na Shirika la Kazi Duniani (ILO)kupitia mradi unaofadhiliwa na United Nations Partnership on the Rights of Persons with Disabilities (UNPRPD) wenye lengo la kukomesha unyanyapaa na ubaguzi wa watu wenye ulemavu katika vyuo vya ufundi na kazini.  Katika majadiliano hayo, Wadau wameweza kutoa maoni yao na namna bora ya hatua za kuchukuliwa ilikufikiwa malengo, h...

TMDA YANG'ARA MASHINDANO YA SHIMMUTA, YAICHAPA LGTI MABAO 4 KWA 2.

Image
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. TIMU ya soka ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) maarufu kama TMDA FC imeicharaza timu yaChuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo ya LGTI FC kwa jumla ya mabao 4 dhidi ya 2 katika mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea Jijini Dodoma. Mchezo huo umechezwa leo saa 2:00 asubuhi katika uwanja wa Humanity-1 uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma. Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa TMDA Bw. Brian Kyando ameeleza kuwa timu yake ilijiandaa vyema kupata matokeo katika mchezo huo. "Tunamshukuru Mungu kwa kupata matokeo mechi ya leo.  Tulijipanga kushambulia kuanzia dakika ya kwanza ili tuweze kupata magoli mengi lakini wapinzani wetu nao walijitahidi kutuzuia tukaishia magoli hayo manne. Mchezo huo umeshapita na sasa tunaangalia michezo iliyo mbele yetu ili nayo tufanye vizuri. Mashindano ya SHIMMUTA yameanza kuanzia tarehe 12 Novemba, 2023 na yanatarajiwa kuendelea hadi tarehe 25 Novemba, 2023.