Posts

MATOKEO DARASA LA SABA 2024.

Image
  NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2024 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU SONGWE

DAKTARI KIZIMBANI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 12 BUKOBA.

Image
  Na Alodia Dominick, Bukoba Daktari wa viungo Haruna Ayubu maarufu kama Rubai (63) mkazi wa kata ya Rwamishenyi manispaa ya  Bukoba amepandishwa kizimbani kwa shitaka la ubakaji wa mtoto wa miaka 12. Rubai amefikishwa katika mahakama ya wilaya Bukoba Oktoba 23 mwaka huu na kusomewa kesi ya jinai namba 30251/2024. Upande wa mashtaka unaongozwa na mawakili wawili ambao ni Matilda Assey pamoja na Alice Mutungi. Akisoma maelezo ya awali wakili upande wa mashtaka amesema kuwa, kati ya Desemba 2023 na Oktoba 19, mwaka huu  mshitakiwa amekuwa akimuingiza mhanga katika moja ya chumba katika ofisi yake iliyopo mtaa wa Pwani, kata ya Miembeni manispaa ya Bukoba. Assey ameeleza kuwa, alipoingia katika chumba hicho alimvua mhanga nguo zake za ndani kisha na mshitakiwa kuvua nguo zake na kuchukua uume wake na kuuingiza kwenye uke wa mhanga baada ya mshitakiwa kumwingilia au kumbaka mhanga amekuwa akimpatia sh. 10,000 au 5,000 kwa ajili ya kuwapelekea wazazi wake. Aidha amesema, Oktob...

TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO KUZINDULIWA TAREHE 23 OKTOBA 2024

Image
  Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Tamasha la sanaa Bagamoyo, leo tarehe 22 Oktoba 2024. katika ukumbi wa TaSUBa mjini Bagamoyo. ................................. Na Athumani Shomari Mkwama. Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linatarajiwa kufunguliwa rasmi Tarehe 23 Oktoba 2024 katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa TaSUBa mjini Bagamoyo, Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wamejipanga kupokea wageni na kuwaburudisha kutokana na burudani za sanaa na utamaduni zitakazowasilishwa kwenye Tamasha hilo. Amesema TaSUBa imekuwa ikifanya tamasha kama hilo kila mwaka na kwamba kila mwaka linakuwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita na mwaka huu pia litakuwa bora zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita. Am...

MTAALAMU BINGWA WA NYONGA NA MAGOTI KUTOKA UINGEREZA AWASILI DAR.

Image
Atashirikiana na wataalamu wa Mloganzila Na Mwandishi Wetu MTAALAMU bingwa wa upasuaji wa nyonga na magoti  kutoka hospitali ya Queen Elizabeth ya Uingereza Profesa Mamoun AbdelGadir, amewasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya kambi ya matibabu ya siku tano kwa watanzania. Daktari huyo kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani atafanya upasuaji huo kwenye kambi itakayofanyika katika hospitali ya Muhimbili Mloganzila  kuanzia Jumatatu 21,Oktoba 2024. Aliwasili leo  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo alipokelewa na wafanyakazi wa Global Medicare ambao wameratibu kambi hiyo kwa kushirikiana na Muhimbili Mloganzila.  Akizungumza kwenye mapokezi hayo, Meneja Mkuu wa Global Medicare, Daniel Lazaro,  alisema wamefurahi kuona amefika salama nchini Tanzania na kwamba ujio wake utakuwa wa manufaa makubwa kwa watanzania wenye matatizo ya nyonga na magoti. “Tumefurahi kuona umefika salama na tunatarajia watanzania wengi watanufaika na ujio wako kwenye...

TRA KAGERA YAWAPA ELIMU YA KODI WAANDISHI WA HABARI.

Image
  Afisa uhusiano mkuu kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga, akizungumza katika mafunzo hayo. .............................................. Na Alodia Dominick, Bukoba Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) nchini imeendelea kusisitiza wananchi wanaponunua bidhaa yoyote kudai risit na wanapouza kutoa risit kwa kufanya hivyo pande zote zitakuwa zimechangia ulipaji kodi inayosaidia katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Afisa uhusiano mkuu kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga ameyasema hayo Oktoba 19,2024 wakati akizumgumza na waandishi wa habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka hiyo. Kamoga amesema, waandishi wa habari ni sehemu ya kuchochea maendeleo ya nchi yao na wanao wajibu wa kuelimisha jamii juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulipaji kodi kwani asilimia 70 ya mapato ya serikali inatokana na kodi huku asilimia inayosalia ikitokana na wahisani mbalimbali. "Unaponunua bidhaa ukadai risit unatimiza wajibu wako, risit ...

HOSPITALI YA SHIFAA YAZINDUA KITUO CHA TIBA NA UTAFITI WA SARATANI DAR

Image
  Picha mbalimbali wakati Waziri wa Afya,  Jenista Mhagama alipozindua kituo cha tiba na utafiti wa saratani katika hospitali ya Shifaa iliyoko Kinondoni barabara ya Msese jijini Dar es Salaam Ijumaaa Tarehe 11 Oktoba 2024. ....................................... Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama amezindua Kituo cha Tiba na Utafiti wa Saratani cha Shifaa na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuongeza bajeti ya dawa za saratani kila mwaka kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani. Waziri Mhagama aliyasema hayo Ijumaa jioni jijini Dar es Salaam wakati akizindua kituo hicho kilichopo kwenye hospitali ya Shifaa barabara ya Msese Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alisema wakati idadi ya wagonjwa ikiongezeka wagonjwa wengi wanaougua ugonjwa huo hawana uwezo wa kugharamia matibabu hivyo wanahitaji kusaidiwa. Alisema kwa mwaka huu wa fedha pekee serikali imetenga shilingi bilioni 10 kwaajili ya kununua dawa za saratani na kwamba kila bajeti mpya kiasi hicho kitaku...

WANANCHI 10,378 WAFIKIWA NA HUDUMA YA AFYA YA MACHO LINDI.

Image
NA HADIJA OMARY, LINDI. Jumla ya Wananchi 10,378 kutoka halmashauri sita za Mkoa wa  Lindi  wamefikiwa na huduma ya Afya ya macho ambapo kati yao 9690 wamefanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu  Hayo yameelezwa na Dokta Sharifu Hamza kwa niaba ya Mganga Mfawidi wa hospital ya Rufaa MKoa wa Lindi Sokoine, Jana oktoba 10 wakati wa maadhimisho ya Afya ya macho yaliyofanyika kimkoa Katika hospital hiyo ya Rufaa Sokoine huko Manispaa ya Lindi . Zoezi hilo la utoaji Elimu ya Afya ya macho sambamba na vipimo na matibabu limeendeshwa kwa ufadhili wa mashirika ya  Heart to Heart foundation,  CBM pamoja na Korea church . Amesema  zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku saba kuanzia oktoba 4 hadi 10 wataalamu walipita katika shule mbalimbali kwa halmashauri zote sita kutoa elimu pamoja na kutoa matibabu kwa wananchi walioonekana na changamoto ya afya ya macho. maadhimisho hayo ya Afya ya macho  yanayohimiza vijana na watoto kupenda macho yao na  kuitaka dunia kuonge...