Posts

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ASEMA HAJARIDHISHWA NA MKANDARASI WA REA III WILAYANI KILOLO

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uwominyi wilayani Kilolo mkoani Iringa juu ya mikakati ya serikali ya kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme. .............................. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amebainisha kutoridhishwa na namna Kampuni ya Mkandarasi Sengerema inavyotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza na kuitaka hadi ifikapo Desemba 15 kuwepo na mabadiliko ya kazi walizofanya katika Wilaya ya Kilolo. Mgalu ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Alisema Serikali ilishatoa maelekezo na walikubalina na wakandarasi kuhakikisha kila wiki wanawasha umeme katika vijiji 3 na kampuni ya Sengerema imepewa kazi ya kufikisha miundombinu ya umeme katika vijiji 145 Mkoa mzima na kwa Kilolo ni vijiji zaidi ya 40. “Muda umebaki mchache wa kukamilisha miradi hii maana inatakiwa kumalizika Juni mwakani, huku tukiwa tunash...

WAKUU WA MIKOA, WILAYA NA WAKURUGENZI SIMAMIENI UWAJIBIKAJI-MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita  kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. Kulia ni Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ................................. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wahakikishe wanasimamia vizuri uwajibikaji na utowaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao bila ya woga.  Kadhalika, Waziri Mkuu amemtaka kila mtumishi wa umma nchini awajibike katika kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu, wavivu  na haitosita kuwachukulia hatua. Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na watumishi, viongozi wa mkoa, wilaya ya Geita na taasisi za umma ka...

DC BAGAMOYO AGAWA SUKARI YA MAGENDO KWA SHULE, MAGEREZA NA VITUO VYA KULELEA WATOTO.

Image
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akipokea Sukari kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha Bandari ya Bagamoyo, Raymond Mwanisawa.   Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa, akizungumza mara baada ya kupokea sukari na kuikabidhi kwa wakuu wa shule za serikali. ......................................... Serikali wilayani Bagamoyo imekamata sukari iliyoingizwa kwa njia ya magendo na kuigawa kwa shule za sekondari na msingi, Magereza na vituo vya kulelea watoto yatima na wale wa mazingira magumu. Akizungumza wakati wa kupokea sukari na kuigawa kwa wakuu wa shule, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Zainabu Kawawa alisema wilaya ya Bagamoyo imejipanga kikamilifu kukomesha mianya yote ya kukwepa ushuru na kwamba kila anaejaribu kutumia Bandari bubu sheria itamshugh...

ATUHUMIWA KUTUMIA JINA LA KIKWETE KUKWEPA KODI.

Image
Na Shushu Joel,Chalinze. MFANYABIASHARA mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam Innocent Kimaro ambaye anajihusisha na uuzaji wa madini ya mawe aina ya Dolomite ambayo hutumika  viwandani kwa ajili ya kutengenezea Vigae katika wilaya ya Bagamoyo Halmashauri ya chalinze mkoani Pwani anatuhumiwa kutumia jina la mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kwa ajili ya kukwepa kulipa kodi na kupitisha mizigo yake bure kwa kuwatishia wahusika wa kulipisha ushuru. Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji cha msoga Ramadhani Mrisho ambapo mawe hayo yanachimbwa  alisema kuwa mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina la Innocenty Kimaro amekuwa akikataa kulipa kodi pindi anapopitisha mizigo yake kwenye mageti  kwa kudai kuwa yeye ni mtu wa karibu na mbunge wa jimbo hilo (Ridhiwani Kikwete) hivyo si sahihi yeye kulipa kodi kwenye eneo hilo. Aliongeza kuwa magari yake yanaposimamishwa kwenye mageti ili aweze kulipa ushuru madereva wake wamekuwa wakikaidi kusi...

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 28, 2018

Image

NAIBU WAZIRI KILIMO MGUMBA ATOA ONYO KALI KWA MADALALI

Image
Naibu waziri Omary Mgumba akiongea na wakulima wa kijiji cha ngulwe Naibu Waziri Mgumba akikagua maghara ya kuhifadhia mbolea mkoani Iringa ........................................ Naibu waziri wa Kilimo Omari Mgumba Ametoa Onyo Kali Kwa Madalali Wanaowauzia Wakulima Wa Mazao Ya Chakula Na Biashara Mbolea Kwa Bei Ya Shilingi Elfu sabini, 70,000 Badala Ya Kufuata Bei Elekezi Ya Serikali Ya shilingi elfu sitini na nne na mia saba, 64,700  Kwa Mfuko Moja. Akiwa Katika Ziara Mkoani Iringa Ya Ukaguzi Wa Upatikanaji Wa Mbolea Kwenye Maghara Ya Serikali Na Wawekezaji Mkoani Hapa Naibu Omar Amewataka Madalali Hao Kuacha Mara Moja Tabia Hiyo Kwasababu Serikali Ya Awamu Ya Tano Chini Ya Rais Magufuli Aina Utani katika Kuwasaidia Watu Masikini Na Wangonge. Onyo ilo limetolewa Baada Ya Wananchi Wa kijiji Cha Ngulwe Wilayani Kilolo Kutoa Malalamiko Yao Wakati Wa Kikao Kilichowahusisha Wakulima Na Waziri Mgumba. “Ndugu wananchi Nimeskia Malalamiko Yen...

WAZIRI JENISTA ATOA SOMO KWA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Taasisi za serikali Sekta Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali  waliojumuika katika uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha. ............................... Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama amewapa somo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuwa mfano katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwapa mwanga wananchi kuona mfano na kuiga na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025. Ameyasema hayo leo mkoani Arusha  alipokuwa akizindua Kongamano la Mwaka liliwakutanisha Wataalam wa Maendeleo kutoka Wizara husika, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Waziri Jenista amesema kuwa katika maendeleo ya nchi yoyote Wa...