NA HADIJA OMARY
LINDI.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Lindi limepitisha mkataba wa makubaliano ya Biashara ya hewa ukaa katika vijiji 10 , jumuhiya za uhifadhi wa Misitu 3 na msitu wa hifadhi wa manispaa na kampuni ya village climate solution limited (VCSL).
Wakizungumza katika kikao cha robo ya tatu ya baraza hilo , madiwani hao wamesema kuwepo kwa biashara hiyo kutaiongezea Halmashauri chanzo kipya cha mapato na kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa Manispaa na wananchi kwa ujumla
Meneja wa Mradi huo yahya Mtonda amesema Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi kisichopungua miaka 40 katika Vijiji vya Kiwawa, Mputwa, Milolo magharibi, Ruhoma, Muungano, Kinyope, Likwaya, na Makumba.
" sambamba na vijiji hivi mkatamba huu umehusisha jumuhiya za uhifadhi wa Misitu ambazo zimeanzishwa pembezoni mwa Mtaa wa Nandambi, pamoja na msitu wa hifadhi wa Makangara katika Manispaa hii ya Lindi nao pia umeingia katika Biashara ya hewa ukaa"
Amesema miongoni mwa sababu ya mradi huo kutekelezwa kwa miaka 40 ni kufanya ulinzi wa Misitu hiyo kwa muda mrefu ili kupunguza hewa ukaa kwa kuhifadi Misitu hiyo ili viweze kuwasaidi vizazi vya sasa na vijavyo.
" ki asili misitu inaweza kuishi kwa muda mrefu hivyo basi kutokana na sababu hiyo basi miti inaweza kuendelea kuruhusu kufanyika kwa biashara hii ya hewa ukaa kwa kipindi hicho cha miaka 40
Kama tutaweza kuwezesha malipo ya fedha zinazotokana na biashara ya hewa ukaa kwa kipindi cha miaka 40 basi fedha zile zitaenda kwenye shughuli mbalimbali za vile vijiji na ni matumaini yetu vijiji vitaenda kukua kwa kuboresha vijiji vyao
Pamoja na kusaidi makubaliano hayo pia Baraza limepitisha mipango na sheria ndogo za uhifadhi wa Misitu kwa kijiji cha Milola, Mputwa na kijiji cha Namtamba baada ya kusaidiwa na shirika la kuhifadhi misitu tanzania TFCG kuanzisha misitu ya hifadhi kwa kufanya matumizi bora ya Aridhi ya vijiji vyao kwa kipindi cha miaka 40.
No comments:
Post a Comment