Na Mwandishi wetu,
Lindi.
Brigedia Jenerali Charles Peter Feruzi amewataka vijana waliohitmimu mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) kuwa wazalendo waaminifu katika kusimamia na kuijenga nchi yao.
Brigedia Jenerali Charles Feruzi ametoa rai hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kujitolea oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 843 huko Wilayani Nachingwea
Amewataka wahitimu hao kutumia Mafunzo waliyoyapata katika kuijenga na kuilinda Nchi kwa kuzingatia kiapo chao.
Pia amewataka kujiepusha na matumizi yasiyofaa katika mitandao ya kijamii na badala yake waitumie mitandao katika kujifunza na kwa manufaa bila kuvunja sheria na Taratibu za Nchi yao.
Luteni Kanali Nyagalu Malecela ni mkuu wa kikosi cha 843 Nachingwea amesema vijana hao wakiwa kambini hapo kwa majuma 16 wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya awali ya kijeshi na kuwajenga vijana hao kuwa wakakamavu pamoja na wazalendo
Awali akitoa salamu za Wilaya katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mabruck Balozi, aliwasihi wahitimu hao kuendelea kujiendeleza kimasomo.
" ni kwa kupitia Elimu kijana unaweza kuwa Meneja wa Benk, Mkuu wa kikosi, Mbunge , Waziri na Hata Rais hivyo niwasihi vijana kujiendeleza kimasomo ili mfikie malengo yenu" alisema Balozi.
Nao baadhi ya wahitimu wakaeleza umuhimu wa mafunzo hayo sambamba na kuwasihi vijana wengine kujiunga na jeshi hilo
No comments:
Post a Comment